Sunday, November 27, 2011

Utegemezi. . . .

Utakuwaje tegemezi?

1.Kwa kukosa maarifa na msukumo wa kujituma. . .
Unakuta mtu hajasoma hivyo inakua ngumu kupata kazi inayorequire kisomo. . . zile za kawaida na ujasirimali anapuuza maana hapendi kujituma.
2.Malezi na mazoea. . .
Kuna watu katika kulelewa kwao walizoe kila kitu kinatoka kwa baba/mama mpaka umri ambao ni mkubwa sana.Yani wanaendekezwa. . . sasa ikitokea yule mzazi hayupo tena au hana uwezo wa kumpa mahitaji yake mtoto (ambae ni mtu mzima sasa) anatafuta pengine pa kutegemea maana hakufunzwa kujitegemea.Watu hua wananyanyasika kweli kwa hii hali. . . ndio maana ni muhimu kuwafundisha watoto kujitegemea kihisia. . . kimatendo na kimawazo.
3.Kutokujiamini. . .
Hii inaweza kuzaliwa namba mbili hapo juu. . . au ikawa tuni matokeo ya low-self esteem and morale.
4.And then there is the Dependent Personality Disorder. . .
Unakuta mtu yeye kama yeye haamini kwamba anaweza kujitosheleza mwenye (emotionally. . financially. . .au hata kimawazo) Yani lazima ategemee watu wengine. . . hivyo ndivyo alivyojengeka.

Binafsi naamini kwamba utegemezi ni ugonjwa mbaya zaidi ya ukoma. . . mbaya zaidi kwa kuwa tegemezi ni sawa na kujiweka mahabusu.Unakosa uhuru wa kufanya yale unayopenda na kuamini. . . unakosa kuheshimiwa. . . unakosa ujasiri wa kusimamia yale unayoona unastahili. . . unashindwa KUWA WEWE na kujikuta unakua yule watu wanaotaka uwe kwasababu unawategemea.

Kama wewe ni tegemezi (hisia zako. . matumizi yako. . .mawazo yako na maisha yako kwa ujumla yanaendeshwa na mtu/watu wengine) anza kuachana na hiyo tabia.
1.Anza kuwa na na mawazo yanayojitegemea.
Usikubali kupelekeshwa na mawazo/imani za watu wengine.Kuwa tofauti na watu wenginesio kosa na wala sio vibaya as long you are not hurting anyone.Let people agree to disagree with you.
2.Jitume.
Kama ni mama wa nyumbani anzisha bustani au kabiashara kako kadogo.Fuga kuku uza mayai. . .nunua mboga mboga za jumla uza mtaani kwako.Yani hakikisha chumvi ikiisha huendi kukopa na kusubiria baba nanii aje umuombe sh.300. Kwa wanaume vile vile. . . yawezekana mkeo ndio mwenye kazi/kipato kikubwa. . . wewe hakikisha tu unatoa mchango wako nyumbani. . . hata kama ni mdogo.
Kama ni binti. . .pangilia pesa ya matumizi unayopewa kama vile umetoka kuifanyia kazi naunaionea uchungu.Jifunze kujipa unayohitaji kabla ya unayotaka kukwepa mitego.
3.Fanya wewe ndio uwe mwamuzi mkuu wa nini kinachoendelea maishani mwako.Kwepa kuwapa watu wengine fursa ya kukuendesha. . . wewe ndo unatakiwa uwe dereva.Ukikata kona unakata kwasababu ndicho ulichotaka na sio ulicholazimika kufanya.

Ila ushauri wangu mkuu unaenda kwa wazazi na walezi ili wadogo zetu nao wasije wakaanguka kwenye dimbwi la kuwa wategemezi.
1.Jitahidi kumpa mwanao/nduguyo elimu ya darasani pia ya maisha.Akifaulu yote atakua na mafanikio kimaisha na kiakili.
2.Mruhusu/mfundishe kujieleza pale mnapokua mmepishana badala ya kusema tu "wewe ndie mwamuzi". . . hata kama ni kweli reason with him/her ili aelewe kwanini.Hii itamsaidia kuwa na mawazo yanayojitegemea badala ya kuwa bendera fuata upepo.
3.Mfundishe kusimamia kile anachoamini as long as hatendi kosa.
4.Mfundishe kujituma. . .mpe kazi ndogo ndogo hata kama mna mfanyakazi/ wafanyakazi.
5.Mjengee kujiamini.
6.Hii inashirikiana na namba nne na ntaitolea mfano.Mfundishe THAMANI YA PESA.Ndio inawezekana uwezo unao wa kumnunulia kila atakacho ila kwa kufanya hivyo hutokua unamsaidia maana mbeleni hayo mazoea yatakuja kumsumbua.

Mfano. . .badala ya kutengewa chakula mezani na kuondolewa nvyombo. . .kutandikiwa kitanda na kusafishiwa chumba chakulala anaweza akafanya hizi shughuli mwenyewe. It only takes a couple of minutes a day. . ila somo lake litadumu maisha.Nakumbuka sisi nyumbani tulikua na sheria. . .ukila/kunywa kitu bila watu wengine lazima usuuze vyombo utakavyochafua.Vyombo vyote vilikua vinaoshwa na mtu mmoja baada ya milo ya pamoja tu.
Pesa tulikua tunapewa allowance kila mwezi. . .bila masharti.Ila sasa ilikua mtu ukitaka vitu ambavyo sio neccessities (video games,CDs,sijui music players na vikorokoro vingine vya aina hiyo ) unaulizwa kwanza una sh. ngapi. Tulikua tunatakiwa tusave atleast nusu ya bei ya hicho tunachotaka alafu tuongezewe nusu.Au unakopa na kukatwa kwenye allowance inayofuata.
Hii kitu ilitufanya tuwe tunaheshimu vitu vyetu na kujiuliza mara mbili mbili "do I really need/want this" kabla ya kununua kitu.It helped. . .maana mpaka leo na kesho hua sinunui wala sitaki kitu nisicho na uwezo nacho hata kama nakitamani.
Na mwisho wa siku mtu akiruhusu tamaa imtawale lazima utegemezi umtembelee pale atakapokua hawezi kuridhisha tamaa yake maana kuidhibiti hawezi.


Have a nice weekend.

Nini maana ya kusamehe. . . ?

Ni nini maana halisi ya kusamehe??
Je ukimsamehe mtu unalazimika kuwa karibu yake tena?? Kurudiana kimapenzi kama ndivyo mlivyokua mwanzo?? Kuongea mara kwa mara kama ndivyo mlivyokua mwanzo? Kutembeleana mara kwa mara kama ndivyo mlivyofanya mwanzo??

Nauliza kwasababu mara nyingi nimeona/sikia watu wakisema ''mi nilidhani umenisamehe/umemsamehe'' pale wanapotaka mambo yarudi kama mwanzo/au hata yawe zaidi na kuambiwa kwamba haiwezekani. Ina maana ukimsamehe mtu moja kwa moja unategemewa/una jukumu la kumchukulia/treat kama vile hilo kosa alilofanya halikuwahi kutokea?

Binafsi naamini kwamba kumsamehe mtu ni kile kitendo cha kuachilia (letting go) kile kilichotokea. Kumruhusu awe na amani..na kufungua ukurasa mpya ambao unaweza ukachagua awepo ndani yake au asiwepo na sio kukifuta kabisa alichofanya na kulazimika kurudi mlipokua mwanzo bila mhusika (mkosewaji) kutaka/penda kufanya hivyo. Yani inawezekana kumsamehe rafiki mwizi bila kumkaribisha tena nyumbani kwako...kumsamehe mke/mume/mpenzi cheater bila kurudiana nae tena..kumsamehe ndugu/rafiki mmbea bila kumshirikisha mambo yako tena. I don't know...inawezekana kwa kufanya hivyo mtu anakua hajasamehe ila ndivyo nnavyoamini na kufanya pia...hata mimi siwezi lazimisha/taka/tegemea mtu niliyemkosea na akanisamehe kurudisha mahusiano yetu ya mwanzo kwasababu tu ameniambia ''NIMEKUSAMEHE''.Ntategemea anipotezee/awe karibu na mimi kwasababu anapenda/taka kufanya hivyo na sio kama jukumu linalofuatana na msamaha wake.


Nilipost hii mada JF wiki kadhaa zilizopita tukawa na majadiliano mazuri kweli . . . tembelea hii link kufuatilia mjadala http://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/195263-nini-maana-ya-kusamehe

Apologies. . . .

Finally I can write again on my own terms.

My laptop and cellphone died so I couldn't write out of school and that's why I haven't been able to post anything but now I can.I just have to finish my writting assignments so I can pay more attention to the blog.

Nisameheni kwa kuwaweka bila kitu and thank you for sticking around.

Much love.
LIS

Sunday, October 30, 2011

Wakatisha tamaa...DOWNERS!

Downers....
...That's what I call the people that are constantly trying to put others down.

Watu kama hawa wako kila mahali, majumbani, mashuleni, makazini na hata mitaani.Wanawashushia wenzao ari ya kusoma, kutafuta maendeleo, kufanya kazi, kukuza na kuendeleza vipaji vyao kwa sababu ya madhaifu yao wenyewe au woga wa kuwaona wengine wakifika mbali.

Muda sio mrefu nilitokea kuangalia kipindi cha mashindano ya kuimba, kabla ya kuimba dada mmoja (umri miaka 37 kama sikosei) akawa anaelezea kwanini imemchukua muda mrefu kujaribu bahati yake. Alikua na mpenzi ambae kila akiimba alikua anamwambia hana sauti nzuri na maswala ya kuimba hayawezi kumfikisha popote kwasababu hana kipaji. Dada wa watu alisikia hayo maoni so many times mpaka na mwenyewe akaanza kuamini kwamba ni kweli hana kipaji japo wakati anakua aliamini anacho. Akapoteza kujiamini mpaka alipokuja kuachana na yule bwana na ndio akaona aende kwenye hayo mashindano.
Honestly yule dada alipoimba tuchozi tulinitoka....pamoja na watu wengine wengi tu waliokuwepo kweny hicho kipindi.Her voice was simply AMAIZING.....

Wapo watu wengi sana wanaonyang'anywa kujiamini kwa namna hii..wakubwa kwa wadogo.Wakati mwingine hata mzazi anaweza akachukua nafasi hiyo ya kumshusha mwanae...yaweza isiwe kwa makusudi bali kwa yeye kuamini kwamba mwanae hawezi hicho anachojaribu ila inatokea na inaathiri.


So next time ukisikia mtu anakwambia ''huwezi hichi...huwezi kile'' usichukulie hayo maneno kama sheria. Usikubali kuaminishwa huwezi wakati unaweza...hutofika mbali wakati matumaini yapo...WASHANGAZE watu waliodhani hutofika, hutoweza kwa kupigania na kufikia malengo yako.

Jifunze kutofautisha criticism na discouragement.
..Criticism imejikita kwenye kujenga na kuboresha zaidi. Kukupa moyo na kukuimarisha...UKIPEWA CHUKUA NA TUMIA VIZURI KWA FAIDA YAKO.
..Discouragement imejikita kwenye kubomoa msingi wa kujiamini kwenye mambo au jambo fulani. Kukuonyesha kwamba huwezi na hata ufanye nini hutoweza .HII USIRUHUSU IKUTAWALE.

Kama wewe ni mzazi...jitahidi kumkosoa mwanao pale inapobidi ili kumjenga (critisism is good ) ila usimkatishe tamaa.
Kwa wengine wote....usiruhusu madhaifu yako...kutokujiamini kwako...chuki...wivu au hata mtazamo wako kuhusiana na maisha uathiri watu wengine. Kosoa kwa nia ya kujenga ...kama huwezi acha!!

Be blessed....and stay blessed.
LIS

Friday, October 28, 2011

Zawadi sehemu ya 7

Poleni kwa kusubiria sana mwendelezo.....

Kwa dakika nilitamani ningekua na uwezo wa kusoma mawazo ya baba nikajua nini kilikua kinaendelea kichwani kwake .Maana aliyofanya pale wodini yalikua nje ya matarajio yangu kabisa na hata nilipojaribu kufikiria nini kilichosabisha kile nilichoshuhudia sikufanikiwa. Nilidhani labda amechanganyikiwa, lakini hakuonekana kama mtu aliyechanganyikiwa bali mtu mwenye hasira zisizodhibitika.

Pamoja na kwamba baba hakusema neno baada ya zile purukushani hasira zake haziokuonekana kupungua. Wale waliomshika walimuomba watoke nje kidogo nae hakukataa. Akanitazama kwa jicho kali kisha akaongozana nao na kutoka nje ya wodi tuliyokuwamo. Kitendo cha kubaki pale chumbani mwenyewe hakikunipa unafuu bali kilinifanya niogope kile kilichokua kikiendelea. Nilitamani mtu mwingine aje mle ndani ili nijuzwe kilichokua kinaendelea ila haikua hivyo. Mawazo ya kuchomoa dripu niliyokua nimechomekewa mkononi mwenyewe ili nitoke nje yalinijia ila sikuthubutu.

Wednesday, October 19, 2011

Ukishikwa.....

........shikamana!


Inashangaza kweli wakati mwingine jinsi watu wanavyoBEHAVE kwenye mahusiano.Wengine utakuta wanaendekeza KIBURI...wengine KUDEKA...wengine KULALAMIKA...KUGOMBA kila saa n.k tena bila sababu ya msingi.

Vyote hivi vikizidi kwakweli vinaweza kuvunja mahusiano maana INABOA/CHOSHA...kuna mtu unakuta hata akikosea yeye samahani mwiko.Hata ukimuwia mpole japo ye ndo mwenye kosa inakua bado haitoshi....yani kiburi chake ndo kinamtawala.
Wale walalamikaji nao yani utadhani ulimwengu mzima kabebeshwa yeye....kila saa kama anataka kulia..kila kitu ye ni kama anaonewa.Hata akifanya kosa kulia atalia yeye ...na kubembelezwa atabembelezwa yeye.Hawa wadekaji maarufu ndo kabisaaa...mtu kadri unavyombembeleza ndivyo anavyozidisha!Yani utadhani mashindano...mpaka mwisho wa siku mtu unaamua kumpotezea tu!

Nnachosema ni kwamba...mapenzi sio kukomoana jamani!Kila kitu fanya kwa kiasi!Wapenzi/wenza hawatakiwi kua na ushindani...labda kama mnashindana kuonyeshana mapenzi na sio nani kinara wa kulalamika au nani mwenye kiburi zaidi ya mwenzie!Hivyo basi ukishikwa shikamana...ukielezwa elewa...ukipendwa pendeka...ukiheshimiwa heshimu na heshimika pia!

Be blessed and stay blessed!
L..I.S

Favorite shots...BARCA!

''Un vaso de vino tinto por favor''
That was my very first full Spanish sentence in Spain...i'll probably never forget it..EVER.

One of the streets on a Saturday morning...really quite!!

Spotted this lil' beauty outside the hotel and we just had to take a picture.


I forgot the name of this place but it;s some kind garden with a lot of beautiful statues and fountains in it.Really nice...the weather was hot but being in the garden felt amazingly cool! 
Waiting for a TRAM after a long day of touring around the city and the Barcelona's national stadium.
Ohhhh and I think the TRAM is like one of the coolest way transportation ever invented....will attach a pic .

After climbing a couple of flights up I was exhausted...but the view of the city from up there was certainly worth the climb.
And there is a tram......

I'm back...

Hi guys...

...sorry for abandoning you AGAIN.
My laptop was down and my phone is dead (water damage)so It was kind of hard for me to post new topics. But honestly....even if my stuff were working I probably wouldn't have written much anyway because I have being feeling Uninspired lately, which lowers my creativity level.

Anyway I finally got inspired today so let me put it to use before y'all lose interest on my blog!!
Stay tuned......

Ohhh and by the way..I LOVE PHOTOGRAPHY.
Being behind a camera or in front of it is something I absolutely enjoy doing. Pictures are perfect when it comes to triggering memories and imagination , inspiring (like what happened to me today) and rewarding emotionally. So I’m gonna have a new session which will be called FAVORATE SHOT(S) at least twice a week... I hope you guys will enjoy it.

Be blessed and stay blessed.
L.I.S

Saturday, October 8, 2011

A blessing....


Looking at your beautiful face...
Being in this time and place...
I feel so blessed!!
And I thank God for he's given me the best!

You eyes so bright..
Spreading such light..
I wonder...is this real?
Is it right for me to feel the way I feel?

Yes!!I was unsure once..
When I was left with not much of a choice...
Looking at my options...

 I had to choose with caution and make the right decision.

I did right...
I won the fight...
Now all I got is a smile on my face


Now my beautiful one, on this beautiful day
I wish you a happy birthday
A beautiful life with a lot of success
Many blessings and NO stress

I LOVE YOU!

Be blessed and stay blessed!
L.I.S

Sunday, October 2, 2011

Wazazi wenza.....

Linapokuja swala la mahusiano/ndoa na watoto waliozaliwa kabla hua hatuachi kuongelea mama wa kambo na malezi ya watoto.Napenda kuongelea wamama tu maana wababa wengi hua hawana matatizo wawe wazazi kabisa au walezi(wale wa kambo) linapokuja swala la mzazi mwenza kua na mahusiano mapya au wale wa kambo kulea watoto wa mwenzie tofauti na wa mama!


Nwy mara nyingi wasiwasi hua unakua kwa watoto zaidi na malezi/uwepo wa mama wa kambo.Tunasahau kwamba hata yule mwanamke mpya anaweza akanyanyasika na uwepo wa watoto wasio wake pamoja na mama yao bila kusahau ndoa yake kuyumbishwa kama mti usio na nguvu dhidi ya upepo.Kama tunavyojua wakati mwingine au niseme baadhi ya wanawake hua na vinyongo..gubu..chuki kwa wazazi wenzao kwa kuachana nao...na kitendo cha mwanaume kupata mwanamke mwingine na kuoa hakiwi cha furaha kwa wote!Sasa wanawake wa aina hii wanaweza kutumia watoto wao kuyumbisha ndoa ya wengine pia kusambaza chuki.Ila muhimu hapa ni hili la kuyumbisha ndoa...kuharibu au hata kuondoa kabisa amani ndani ya nyumba ya mwanamke mwingine kwa kutengeneza mazingira ya kuwachanganya wapendanao!

Mzio (allergy) kwa watoto.

Njugu (karanga, korosho, almonds, walnuts, pecans)ni vitu ambavyo watoto wengi wanakua sensitive navyo hivyo kusababisha mzio kirahisi.
Ili kuepuka kugeuza haka kauso kuwa ......
.......hivi unashauriwa kuwa mwangalifu pale unapompa mtoto mdogo vitu ambavyo ndo anakula kwa mara ya   kwanza.Tukirudi kwenye vitu vya jamii ya njugu ni vizuri kumwonjesha mtoto mwenye miaka mitatu na kuendelea na sio chini ya hapo. 

Ikitokea akawa allergic na kitu baadhi ya dalili za haraka unazoweza kuziona ni kuvimba , kuwashwa uso/macho/pua /koo, upele, kupiga chafya, kukohoa, kutapika, kupumua kwa shida  na hata kuzimia. If the reaction is too strong it might kill you kwahiyo ni vizuri kuwasiliana na mtaalamu au kwenda hospitali kabisa ili kupata matibabu yanayotakiwa.

Sina uhakika kwa hapa kwetu inakuwaje ila kwa wale waliopo nchi za magharibi unaweza ukafanya ALLERGY TESTING kujua ni vyakula au vitu gani visivyopatana na mwili wako.......kwahiyo kama uko kwenye nafasi ya kufanya hivyo fanya hivyo ili kuepuka matatizo hapo baadae.

Be blessed and stay blessed.
L.I.S

Poleni na asanteni!

Gosh i'm so glad September is over....it was not a good month at all.

Mambo mengi sana yameenda ndivyo sivyo mwezi huu uliopita kwakweli....nwy poleni kwa kuwaacha solemba ila sasa nimerudi kwa kasi na nguvu za kutosha kuwahabarisha na kuwaburudisha.

Uzuri wa mwezi huu uliopita ni kwamba nimepata hobby mpya na njia ya kutuliza akili...KUFUMA.Ilinichukua angalau masaa kumi kufuma scarf yangu hapo juu ila haikunichosha kabisa.Nadhani ntaendelea nayo mpaka niwe mtaalamu haswa.

Kuhusu ZAWADI (maana najua wengi ndo mnaemsubiria) naomba mnipe muda kidoooogo nimelizie kazi za shule alafu ntaendelea na simulizi yake. Asanteni kwa kunitembelea...

Be blessed and stay blessed.
L.I.S

Saturday, September 10, 2011

Hello....

Hi guys!

Sorry for abandoning you this weekend.

Nilikua nimepanda ntaendelea na simulizi ya Zawadi ili msisubiri sana ila kwa bahati mbaya kikatokea kitu kilichoninyima muda na umakini wa kufanya hivyo.
Ila kilichotokea kimenipa wazo ambalo sikua nimefikiria mwanzo hivyo natumaini na nyie mtafaidika na nilichojifunza...ntawajulisha ni kitu gani kesho maana hata kuambatanisha picha siwezi hapa nilipo.

Poleni tena kwa msiba mkubwa uliotokea Nungwi.

Be blessed and stay blessed!
LIS

Ajali ya meli Nugwi...

Well kwasababu habari tayari imesambaa kila mahali mi naomba niwape tu pole walionusurika pamoja na wale wahusika wa karibu kabisa wa wale ndugu zetu waliopoteza maisha.

Naomba Mwenyezi Mungu awajalie nguvu na ujasiri wa kuweza kupambana na kipindi hichi kigumu.

Ndugu zetu waliopoteza maisha namwomba Mungu awarehemu na kuzipumzisha roho zao mahali pema peponi.
Amen!

Kwa taarifa zaidi tembelea
http://issamichuzi.blogspot.com/
pia http://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/171250-meli-yazama-ikelekea-pemba%3B-wengi-wahofiwa-kupoteza-maisha.html#post2475033

Wednesday, September 7, 2011

Zawadi sehemu ya sita...

''Zawadi, Zawadiiii'' ndio maneno yaliyoniamsha asubuhi ya pili.Nilifumbua macho yangu taratibu na kivivu ili kujua aliyekua ananiamsha ni nani. Mama alikua ameinama akinitazama usoni huku mkono wake mmoja ukiwa umenishika begani.
''Mama, shkamoo.'' nilimsalimu kwa sauti ya chini huku nikifumba macho yangu tena. ''Marahaba mwanangu, unaendeleaje?'' aliuliza bila kuondoa mkono wake begani mwangu. ''Nafuu mama! Umekuja na baba?'' swali hilo lilinitoka kabla sijayafumbua macho yangu na kuyaangaza mle chumbani kuona kama baba alikuwapo.
'' Nimekuja nae ila yupo hapo nje anaongea na sijui ndo mwalimu wako yule.Alafu ilikuaje yeye ndo aliyekuleta hospitali , mashoga zako nao wako wapi?'' japo aliuliza kwa sauti ya utaratibu kama kawaida yake nilihisi shauku ya udadisi ndani yake. Nilifikiria kwa sekunde kadhaa nimjibu nini kisha nikamjulisha kwamba niliwaomba watangulie tulipotoka shule na ningeungana nao baada ya kuongea na mwalimu kuhusu mitihani tuliyokua tukitarajia kuanza jumatatu, na nilipokua naongea na mwalimu ndipo nilipoanguka. ''Ahhhh ndo matatizo ya kutokua na pesa haya. Ungeshatibiwa tangu unaanza kujisikia vibaya haya yote yasingetokea.'' Jibu lake lilionyesha kuridhishwa na langu, ila lilinifanya nijihisi kama mkosaji kwa kumfanya mama ajione kama mzazi asiyeweza kutosheleza mahitaji ya mwanawe, hata pale anapokua mgonjwa. Nilitamani kutoa maneno ya kumfariji ila kabla sijafanya hivyo mlango uligongwa na kufunguliwa mara hiyo hiyo.

Wa kwanza kuingia alikua baba aliyekua amevalia kama ambavyo hua anavaa siku zote akielekea kwenye shughuli zake , kaptula, shati na ndala chakavu kiasi.Bila kusahau kofia yake chakavu aliyotumia kujikinga na jua. Japo kua ilikua imetoboka sehemu kadhaa juu na pembeni bado aliivaa kila siku. Rangi yake ya kijani ilikua imefifia kana kwamba ilikua imedumbukizwa kwenye jiki kwa nia ya kupoteza rangi yake ya awali . Nyuma yake alifuatiwa na mwalimu kisha daktari yule mrembo aliyenihudumia jana yake.
''Hujambo mama?” alinisalimu baba kabla sijatoa shikamoo niliyokua najiandaa kumpa. “Salama tu shikamoo baba!” nilimjibu huku nikimtazama ili niweze kumsoma alikua katika hali gani. Uso wake ulionyesha kuchoka kama ulivyokua wa mama ila alijitahidi kutabasamu hivyo nikajua alikua sawa.
Mwalimu yeye alisimama karibu kabisa na mlango huku akimtazama daktari ambae kwa wakati ule alikua akinipima. “Mrembo naomba uvute hewa ndani kwa sekunde chache kabla ya kuiachia kisha usubiri tena kwa sekunde chache kabla ya kuvuta tena ndani.” maagizo hayo ya daktari yaliambatana na mkono wake mmoja ukisogeza kifaa chake kila kona ya kifua changu upande wa kushoto huku mwingine ukiwa umekishikilia kilipoishia sikioni mwake.
“Mapigo ya moyo yako normal, sasa ngoja niongee na wazee kidogo .Nikirudi nikute bado unapumua ehhhh!!!.” aliniambia mimi uso wake ukiwa umejaa tabasamu lililoonyesha meno yake meupe yaliyojipanga vyema kabla ya kugeuka walipokua wamesimama baba na mama na kuwaomba wamfuate. “Kama hamtojali naomba twendeni ofisini tukaongee kidogo.”