Wednesday, September 7, 2011

Jifunze kusoma alama za nyakati.....!


Kuna wakati unaweza kumkuta mtu yupo kwenye mahusiano yenye kila aina ya karaha na unyanyasaji lakini bado yupo tu na wala hafikirii kuondoka na sio kwasababu hataki bali kwa sababu anakosa ujasiri/msukumo wa kufanya hivyo.Unakuta mtu anatukanwa...anapigwa...anadharauliwa...anasimangwa...yani kwa ujumla anaonyeshwa kila dalili za kuchokwa ama kutotakwa tena lakini anabaki palepale.

Ndio uvumilivu ni muhimu sana kwenye mahusiano...ila pia inabidi tujifunze kusoma alama za nyakati.Kuna vitu ambavyo mwenzi wako akianza kuvifanya tena kwa kuvirudia rudia unatakiwa ujue kwamba hapa sitakikani tena na utafute jinsi ya kujitoa.Ndio maana wahenga walisema ''akufukuzae hakwambii ondoka.'' usisubiri kufukuzwa kama mbwa. Mara nyingi mtu atakufanyia visa akijua kwamba ukivichoka utaondoka mwenyewe...ila sasa kuna wale wenzangu na mie wanaoamini na kujipa moyo wa mabadiliko hata pasipo na nia wala matarajio...unavumilia manyanyaso ukijua kesho itakua bora ya jana alafu matokeo yake jana inageuka bora ya leo pale unapovunjwa moyo kabisa.

Jamani embu tujifunze kusema inatosha na tuache kua ving'ang'anizi.Jiamini kwamba ulivyompata huyo ndivyo ambavyo utampata mwingine.Usiishi kwa mateso, wasiwasi na hofu ya kutokupendwa tena kwasababu hujui kuna kizuri gani kinakusubiria huko nje. Ila sasa hakiwezi kujitokeza bila wewe kuweka hiyo nafasi wazi!Hamna mtu anaestahili kulala akilia kila siku au kutokua na furaha kwasababu ya binadamu mwenzake.Ukiona mtu hakufai achana nae...usimpe mtu mwingine nafasi ya kuyaendesha maisha yako ....hiyo ni kazi yako na yako pekee.Ukitaka furaha itafute....ukikereka na kuchoka huzuni ikimbie!!!



Usisubiri kuvunjwa moyo uokote vipande....ondoka na moyo wako mzima ukatafute atakaeupa furaha na amani!!


So does not matter how much it pains (time heals) ni bora uondoke mapema na kujijenga mwenyewe.., because you should never depend on someone else for your happiness you must be a King/Queen to your own castle so its true "If he cant learn to love you, you should leave him" sababu life is too short and the time you spend na huzuni with someone can be spent better with someone else who know your value.., and they are a lot people out there who will value you more hata kama hakuna ni bora kukaa peke yako kuliko na mzigo wa matatizo........BY J!!

2 comments:

  1. Kweli Kabisa huenda kungagania kwako hapo unakosa baraka na kujinyima raha kama ungeondoka hapo..., mvumilivu hula mbivu lakini kuna mambo hayavumiliki

    ReplyDelete
  2. Thats so true!! Yanini kuendelea kung'ang'ania kwenye uhusiano unaokufanya ulie kila siku?? Ukiona mambo hayaeleweki its better kuondoka na sio kuforce mambo na mwisho wa siku unajikuta kuwa unazidi kupoteza tu na kuwa mtumwa kwa sana!!

    ReplyDelete