Monday, August 29, 2011

Zawadi sehemu ya tano.....



Dakika chache baadae mwalimu alirudichumbani huku akitabasamu.

Uso wake ulionekana kuchangamka hivyokupelekea uchovu na hofu vilivyoonekana kumtawala mapema vijifiche.Macho yake ya rangi ya kahawia yalionekana kutabasamu na midomo yakeiliyochongeka vyema ilionekana kuyaunga macho yake mkono. Kwakumtizama tu ungeweza kutambua kwamba alipenda kufanya mazoezi. Japohakua mwalimu wetu wa michezo karibu kila mara tulipokua na kipindicha michezo alijitahidi kujiunga nasi, na alipendelea zaidi kuchezampira wa miguu kwasababu ulimpa mazoezi ya kutosha. Kwa wakati ulealikua amevalia suruali nyeusi ya kitambaa na shati jeupe la mikonomirefu iliyokunjwa usawa wa viwiko vya mikono yake. Vyote vilimkaasawa sawa kuendana na mwili wake uliojengeka vyema. Urefu wakeuliokaribia sentimita 180 , ngozi yake ya maji ya kunde, mwili ambaohaukuzidi kiasi, macho , pua, midomo na masikio vilivyoutosheleza usowake vizuri vilimfanya awe mwanaume anaevutia kimuonekano.


'' Kimekufurahisha nini?'' nilimuulizapindi alipoingia huku akitabasamu. ''Ahh nimefurahi tu.'' alijibuhuku akitembea kuelekea nilipokua nimelala mimi. Nilipoona vilenilisogea nyuma kidogo kuweka nafasi ili aweze kukaa iwapo angependakufanya hivyo. Nae kama aliyeyasoma mawazo yangu alikuja na kuketipembeni huku mgongo wake akiuelekeza mlangoni hivyo tukawatumetazamana. ''Dah! Mama yako anaonekana mpole kweli, japoulishaniambia leo ndio nimejihakikishia mwenyewe.'' alisema hukuakinyoosha mkono wake wa kushoto upande wa pili ili aweze kugusamkono wangu uliowekewa dripu. ''Vipi kwani?'' niliuliza nikiwa nashauku ya kujua walichoongea na mama. ''Basi tu anavyoongea.Mtaratibu sana, sauti yake tu inajieleza. Anyway alikua nawasiwasi kweli ila nimejitahidi kumuondoa hofu. Alikua anataka kujahospitali sasa hivi nikamwambia kwamba asubiri mpaka asubuhi ilimadaktari nao wawe wamepata majibu ya vipimo. Kaniuliza kama mara nnehivi iwapo naamini utakua sawa , baada ya kumjibu ndio akatuliakidogo.Kwahiyo kesho asubuhi watakuja pamoja na mzee, dah sijui yeyeatakua vipi.'' alipomaliza nilitamani kutabasamu ila nilipomfikiriababa nikaghairi. ''Atakua kawaida tu.'' nilijaribu kumhakikishiahuku nikiomba kimoyo moyo iwe hivyo. ''Kwani we utakuja kesho?''nilimrushia swali bila kua na jibu maalumu nililotaka ama tamanikupata toka kwake. '' I'm not going anywhere, watanikutahapa hiyo kesho.'' jibu lake lilinishangaza kidogo maana sikutegemeakwamba angelala pale, achilia mbali kuwa tayari kuonana na mzeeFadhili asubuhi iliyofuata. Pamoja na kwamba alikua anajua kwambababa na mama walikua hawajui chochote kuhusu kile kilichotokea katiyetu nilitegemea kwamba bado angeogopa kuonana nao uso kwa uso.

Nilifikirianini ambacho kingeweza kutokea iwapo mzee Fadhili angekua anajua,sijui angeanza kumwadhibu yupi kati yetu. Mama sikua na wasiwasi naemaana siku zote alikua mtaratibu na hakuwahi hata kunichapa.Alichoweza ni kunigombeza tena pale tu alipoona ulazima wa kufanyahivyo. Mzee Fadhili nae japo aliwahi kunichapa mara moja tu baada yakupita kwa wenzangu kucheza na kudanganya nilitumwa na mwalimu. Hakuamtu wa kuchezea hata majirani walilifahamu hilo hivyo aliheshimika aulabda aliogopeka kwa wengi.
Kwajinsi nilivyomfahamu baba nilifikiria kwamba labda angeanza na mimikwasababu ndie mwanae, au labda mwalimu kwasababu yeye ndie aliyekuamtu mzima hivyo alipaswa kujua kwamba halikua wazo zuri kua namahusiano na binti mdogo tena ambae bado anasoma. Binafsi nilijilaumumwenyewe kwa kiasi kikubwa kwasababu hakunilazimisha kua nae.Alinivutia na kunipendeza machoni pia moyoni hivyo nikamkubalia, kamakilichotokea siku ile kisingetokea nadhani bado ningeendelea kumuonakama malaika aliyetumwa kunilinda na kunipa furaha maana ndichoalichokua akifanya mwanzo.

''Vipi mbona unaonekana uko mbali sana kimawazo?'' mwalimu aliniuliza.''Basi tu, nafikiria mitihani.Sijui itakuwaje.'' nilimjibu japo sichonilichokua nikifikiria kweli. ''Wala usifikirie sana. Youwill do just fine. Binafsi sinawasiwasi na wewe kabisa, najua utafanya vizuri kama kawaida yako piamarafiki zako wale. Watu wa kuwaonea huruma ni kina Shaban , Zulpha ,Shukuru na washika mikia wenzao.'' kama ada yake alinipa moyo natukaishia kucheka kidogo kwa pamoja baada ya kukumbuka vitukowalivyokua wanafanya shuleni hawa washika mikia. Ni kama vilehawakuja shuleni kujifunza au labda wenyewe walijua kwamba hawawezikujifunza chochote hivyo hawakuhangaika . Badala yake mara nyingiwalikua wakiishia matatizoni kwa yale waliyokua wakiyafanya. Binafsisikuwa na wasiwasi na mitihani hata chembe, nilikua nimejiandaa vyakutosha hivyo niliamini nitafanya vizuri. Nilichoogopa tu ni kuumwawakati wa mitihani, hivyo nilifumba macho na kumwomba Mungu kimyakimya aniepushie mbali hicho kilichokua kinaninyemelea.

Baadae tulisikia mlango ukigongwa na daktari akaingia baada ya mwalimukuitikia. ''Dr. karibu.'' mwalimu alimkaribisha huku akiinuka kutokapale alipokua amekaa na kusimama wima.''Anaendeleaje bibie?''aliuliza huku macho na mikono yake vikiwa bize na dripu niliyokuanimetundikiwa. '' Kichwa kimepungua kidogo ila najihisi mzitokweli.'' ''Hiyo kawaida kabisa. Muhimu sasa upate maji ya kutosha nakitu cha kula alafu upumzike.Sawa? Kesho tutajua kwa uhakika ninikinaendelea kwenye hako kamwili kako.'' wakati anasema hayo hukuakitabasamu mkono wake ulikua tayari ukigusa paji langu la uso .Kusema ukweli sikuwa nimekula kitu tokea mchana ila sikuhisi njaawala hamu ya kula. ''Yeahh unatakiwa ule.Ngoja nikakuangalizie kituhapo nje.'' alidakia mwalimu. ''Mi sisikii njaa bwana.''
nilijibukwa kudeka. '' We siumesikia Dr. alichosema lakini?Unatakiwa ulekitu ili mwili uwe na nguvu.'' kwa jibu lake hilo nilijua sinaujanja. ''Ahhh basi niletee …..uuum ….halfcake na maziwamtindi.'' nilisema nilichoona kingefaa mimi kula kwa wakati ulebaada ya kufikiria kidogo. ''Poa nakuja sasa hivi.'' Waliongozana nadaktari kwasababu nae alikua amemaliza kufanya kilekichomleta.Aliahidi kwamba atamtuma nesi aje kuniangalia tena baadae,na iwapo litatokea tatizo au mabadiliko yoyote yale mwalimuamjulishe.

Mwalimu alirudi akiwa na mfuko mdogo mkononi.Alitoa halfcake mbili alizonunua, maziwa ya mtindi na soda mbili aina ya fanta. Japo sikuagizakitendo cha kuiona pale kilinifanya niitamani hivyo nikamuuliza kamaningeweza kuinywa kwa wakati ule. ''Sure! Nilijua tu utataka maana wewe na fanta utadhani umelogewa .'' alisema hukuakifungua kwa kutumia meno yake kisha akaiweka mezani. Nilitabasamukwasababu ilionyesha ni kwa kiasi gani alikua akinifahamu. '' Sasainabidi uinuke kidogo maana huwezi kunywa ukiwa umelala hivyo.''Alichukua mto mwingine kutoka kwenye kile kitanda cha pili na kurudinao nilipokua mimi.Akaweka mkono wake wa kulia shingoni na kuniuunuajuu kidogo kisha akatumia wa kushoto kuniweke mto mwingine wa ziadauliofanya kichwa changu kiinuke juu bila mimi kuamka. Kwasababusikuweza kutumia mikono yangu yote miwili alinipa soda nikashikamwenyewe kisha akanilisha halfcake moja. Nilipomaliza aliniuliza kamaningependa kuongeza ila nikakataa, akachukua moja iliyobaki naeakala. Baada ya kula tuliongea kidogo, kuhusu nini sikumbuki maanausingizi ulianza kuninyemelea kwa mbali. Kabla sijapotelea kabisaniligundua kwamba mkojo uliokua umenibana muda wote ungenizidia usikuhivyo nilimwambia kwamba nilihitaji kwenda kujisaidia. Akatoka nakurudi na nesi mama mtu mzima aliyefunga ile dripu kwa muda kishaakachomoa ule mrija toka mkononi na mwangu kabla ya kunisindikizauani.Niliporudi akarudisha kila kitu kama kilivyokua kisha akaondoka.

Mwalimu akanibusu kwenye paji la uso kisha nikalala.

1 comment:

  1. What an interesting story! I like it so much, keep it up girl. Without forgetting, your blog is so fantastic,CONGRATS!!!

    ReplyDelete