Showing posts with label zawadi. Show all posts
Showing posts with label zawadi. Show all posts

Friday, October 28, 2011

Zawadi sehemu ya 7

Poleni kwa kusubiria sana mwendelezo.....

Kwa dakika nilitamani ningekua na uwezo wa kusoma mawazo ya baba nikajua nini kilikua kinaendelea kichwani kwake .Maana aliyofanya pale wodini yalikua nje ya matarajio yangu kabisa na hata nilipojaribu kufikiria nini kilichosabisha kile nilichoshuhudia sikufanikiwa. Nilidhani labda amechanganyikiwa, lakini hakuonekana kama mtu aliyechanganyikiwa bali mtu mwenye hasira zisizodhibitika.

Pamoja na kwamba baba hakusema neno baada ya zile purukushani hasira zake haziokuonekana kupungua. Wale waliomshika walimuomba watoke nje kidogo nae hakukataa. Akanitazama kwa jicho kali kisha akaongozana nao na kutoka nje ya wodi tuliyokuwamo. Kitendo cha kubaki pale chumbani mwenyewe hakikunipa unafuu bali kilinifanya niogope kile kilichokua kikiendelea. Nilitamani mtu mwingine aje mle ndani ili nijuzwe kilichokua kinaendelea ila haikua hivyo. Mawazo ya kuchomoa dripu niliyokua nimechomekewa mkononi mwenyewe ili nitoke nje yalinijia ila sikuthubutu.

Saturday, September 10, 2011

Hello....

Hi guys!

Sorry for abandoning you this weekend.

Nilikua nimepanda ntaendelea na simulizi ya Zawadi ili msisubiri sana ila kwa bahati mbaya kikatokea kitu kilichoninyima muda na umakini wa kufanya hivyo.
Ila kilichotokea kimenipa wazo ambalo sikua nimefikiria mwanzo hivyo natumaini na nyie mtafaidika na nilichojifunza...ntawajulisha ni kitu gani kesho maana hata kuambatanisha picha siwezi hapa nilipo.

Poleni tena kwa msiba mkubwa uliotokea Nungwi.

Be blessed and stay blessed!
LIS

Wednesday, September 7, 2011

Zawadi sehemu ya sita...

''Zawadi, Zawadiiii'' ndio maneno yaliyoniamsha asubuhi ya pili.Nilifumbua macho yangu taratibu na kivivu ili kujua aliyekua ananiamsha ni nani. Mama alikua ameinama akinitazama usoni huku mkono wake mmoja ukiwa umenishika begani.
''Mama, shkamoo.'' nilimsalimu kwa sauti ya chini huku nikifumba macho yangu tena. ''Marahaba mwanangu, unaendeleaje?'' aliuliza bila kuondoa mkono wake begani mwangu. ''Nafuu mama! Umekuja na baba?'' swali hilo lilinitoka kabla sijayafumbua macho yangu na kuyaangaza mle chumbani kuona kama baba alikuwapo.
'' Nimekuja nae ila yupo hapo nje anaongea na sijui ndo mwalimu wako yule.Alafu ilikuaje yeye ndo aliyekuleta hospitali , mashoga zako nao wako wapi?'' japo aliuliza kwa sauti ya utaratibu kama kawaida yake nilihisi shauku ya udadisi ndani yake. Nilifikiria kwa sekunde kadhaa nimjibu nini kisha nikamjulisha kwamba niliwaomba watangulie tulipotoka shule na ningeungana nao baada ya kuongea na mwalimu kuhusu mitihani tuliyokua tukitarajia kuanza jumatatu, na nilipokua naongea na mwalimu ndipo nilipoanguka. ''Ahhhh ndo matatizo ya kutokua na pesa haya. Ungeshatibiwa tangu unaanza kujisikia vibaya haya yote yasingetokea.'' Jibu lake lilionyesha kuridhishwa na langu, ila lilinifanya nijihisi kama mkosaji kwa kumfanya mama ajione kama mzazi asiyeweza kutosheleza mahitaji ya mwanawe, hata pale anapokua mgonjwa. Nilitamani kutoa maneno ya kumfariji ila kabla sijafanya hivyo mlango uligongwa na kufunguliwa mara hiyo hiyo.

Wa kwanza kuingia alikua baba aliyekua amevalia kama ambavyo hua anavaa siku zote akielekea kwenye shughuli zake , kaptula, shati na ndala chakavu kiasi.Bila kusahau kofia yake chakavu aliyotumia kujikinga na jua. Japo kua ilikua imetoboka sehemu kadhaa juu na pembeni bado aliivaa kila siku. Rangi yake ya kijani ilikua imefifia kana kwamba ilikua imedumbukizwa kwenye jiki kwa nia ya kupoteza rangi yake ya awali . Nyuma yake alifuatiwa na mwalimu kisha daktari yule mrembo aliyenihudumia jana yake.
''Hujambo mama?” alinisalimu baba kabla sijatoa shikamoo niliyokua najiandaa kumpa. “Salama tu shikamoo baba!” nilimjibu huku nikimtazama ili niweze kumsoma alikua katika hali gani. Uso wake ulionyesha kuchoka kama ulivyokua wa mama ila alijitahidi kutabasamu hivyo nikajua alikua sawa.
Mwalimu yeye alisimama karibu kabisa na mlango huku akimtazama daktari ambae kwa wakati ule alikua akinipima. “Mrembo naomba uvute hewa ndani kwa sekunde chache kabla ya kuiachia kisha usubiri tena kwa sekunde chache kabla ya kuvuta tena ndani.” maagizo hayo ya daktari yaliambatana na mkono wake mmoja ukisogeza kifaa chake kila kona ya kifua changu upande wa kushoto huku mwingine ukiwa umekishikilia kilipoishia sikioni mwake.
“Mapigo ya moyo yako normal, sasa ngoja niongee na wazee kidogo .Nikirudi nikute bado unapumua ehhhh!!!.” aliniambia mimi uso wake ukiwa umejaa tabasamu lililoonyesha meno yake meupe yaliyojipanga vyema kabla ya kugeuka walipokua wamesimama baba na mama na kuwaomba wamfuate. “Kama hamtojali naomba twendeni ofisini tukaongee kidogo.”

Monday, August 29, 2011

Zawadi sehemu ya tano.....



Dakika chache baadae mwalimu alirudichumbani huku akitabasamu.

Uso wake ulionekana kuchangamka hivyokupelekea uchovu na hofu vilivyoonekana kumtawala mapema vijifiche.Macho yake ya rangi ya kahawia yalionekana kutabasamu na midomo yakeiliyochongeka vyema ilionekana kuyaunga macho yake mkono. Kwakumtizama tu ungeweza kutambua kwamba alipenda kufanya mazoezi. Japohakua mwalimu wetu wa michezo karibu kila mara tulipokua na kipindicha michezo alijitahidi kujiunga nasi, na alipendelea zaidi kuchezampira wa miguu kwasababu ulimpa mazoezi ya kutosha. Kwa wakati ulealikua amevalia suruali nyeusi ya kitambaa na shati jeupe la mikonomirefu iliyokunjwa usawa wa viwiko vya mikono yake. Vyote vilimkaasawa sawa kuendana na mwili wake uliojengeka vyema. Urefu wakeuliokaribia sentimita 180 , ngozi yake ya maji ya kunde, mwili ambaohaukuzidi kiasi, macho , pua, midomo na masikio vilivyoutosheleza usowake vizuri vilimfanya awe mwanaume anaevutia kimuonekano.

Zawadi sehemu ya nne....


Sehemu ya nne.........

Siku iliyofuata tulichelewa kuamka kutokana na uchovu wa hadithi za usiku mzima. Aliyetuamsha alikua Jerry aliyetumwa na mama yake kutukaribisha kifungua kinywa. Aligonga mara mbili kabla ya kufungua mlango na kuingia ndani kwa kunyata, pamoja na kwamba tulimsikia wote tulifumba macho kama vile bado tumelala. Alienda moja kwa moja dirishani na kusogeza pembeni mapazia yaliyokua yakizuia jua lililokua linawaka asubuhi ile lisiingie chumbani . Mwanga wa jua ulimmulika Ester aliyekua amelala karibu na dirisha na kumfanya amfokee Jerry kumwomba arudishe mapazia kama alivyoyakuta. “Amka huko acha uvivu. Alafu we ni muongo kweli, jana siuliniambia Zawadi haji wewe?!“ aliuliza Jerry. “Embu ondoka bwana!Au nimwambie mama unatusumbua...!MAMAA!!“ yalikua majibu ya Ester ambae kwa wakati ule hakua tayari kuamka. “Mama mwenyewe ndio kanituma niwaamshe kwahiyo sitoki wala nini.“ nilishawazoea kwa vile ambavyo walikua wakichokozana mara kwa mara, haikua ajabu sababu umri wao haukuzidiana sana hivyo kila mmoja alitaka kumwonyesha mwenzake kwamba hawezi kumtawala.

Saturday, August 27, 2011

Zawadi sehemu ya tatu...


Sehemu ya tatu...

Alinishika mkono wa kulia kwa nguvu na kunivuta ulipokua mlango wa chumbani. Bila kunitazama usoni aliuachia mkono wangu na kunisukuma kitandani , hapo ndipo akili yangu iliporudi. Nilijua nini alichokusudia kufanya na nilihitaji namna ya kuzuia kitendo kile.Kwa haraka niliinuka toka kitandani ili nitoke mbio ila sikupata mwanya huo maana mara hii baada ya kunisukumu alinikandamiza chini kwa mikono yote miwili. Mpaka wakati huo bado sikuelewa mabadiliko yale yalitokana na nini haswa. Macho yake yaliyokua yakinivutia mwanzoni yalinitazama kwa ukali, na kwa mara ya kwanza niliogopa kuangaliwa nayo.
“ Unaniumizaaa“ nililia kwa sauti ya chini. Hakuonekana kujali kwani ndio kwanza alinitazama kwa ukatili. “Malaya mkubwa wewe.“ alisema kwa gadhabu, “Huna shukurani kabisa. Unakula pesa yangu kumbe unaliwa na wengine huko?! Ngoja nikufundishe heshima kidogo“ alisema huku akiwa ameshika shati langu tayari kulirarua.

Machozi yalinitiritika sambamba na sauti ya vifungo vilivyoanguka sakafuni, vilivyogonga ukutani na pia sehemu ya kitanda.Alisogeza uso wake kifuani kwangu kama mtu anaechunguza kitu kisha akaupandisha taratibu.Midomo yake ilipokaribia yakwangu nikafikiria namna ya kumuondoa juu yangu, alipoikutanisha tu yangu na yake nilimng‘ata japo sio kiasi cha kumtoa damu!! “Mamaaa“ alilia huku akiruka kwa maumivu na kujilaza chali pembeni yangu huku akichunguza midomo yake kwa ulimi na mkono wake.Nikatumia mwanya ule kukimbia mpaka sebuleni na moja kwa moja nilielekea mlangoni.Mkono wangu ukiwa umeshika kitasa cha mlango tayari kuufungua nilihisi maumivu makali shingoni. Alinigeuza akanitazama kwa hasira kisha akanikokota tena mpaka lilipokuwapo sofa bila kusema neno. Alinisukuma kisha akanyanyua miguu yangu na kuiweka juu. “Sasa urudie tena ushenzi uliofanya uone ntakachokufanya.Hivi wewe unanijua au unanifahamu?!“ ......“Si nakuuliza wewe?!“ alinizodoa kwa kidole. Sikuweza kujibu maana kilio na kwikwi vilinitawala.