Chakula cha leo ni cabbage.....
Faida zake:
1.Kabichi mbichi inasaidia kutoa uchafu tumboni na kusafisha utumbo wa juu kitu ambacho kinasaidia mfumo wa chakula kufanya kazi vizuri pia kupunguza kuvimbiwa.
2.Inasaidia kuzuia saratani (cancer) hasa saratani ya tumbo.
3.Inachochea mfumo wa kinga kwa kuua bakteria hatari pia inasaidia kupunguza makali ya vidonda vya tumbo.
4..Majani ya nje ni chanzo kizuri cha vitamin E hivyo husaidia kupendezesha ngozi.
Kwa wale ambao hua wanasumbuliwa na tatizo la gas baada ya kula cabbage unaweza ukazisteam/weka kwenye maji ya moto kwa dakika kama tano hivi kabla ya kuzipika.
Kama una matatizo ya goita inabidi ushauriane na daktari kabla ya kula cabbage kwasababu kwa kula cabbage unaweza ukavuruga matumizi ya madini ya chumvi mwilini.
Namna tofauti tofauti ya kuandaa .....
Kupika mboga ..hii nadhani wengi wetu tumezoea na tunaijua.
Pizza salad...hii ni moja ya uandaaji nnaopenda sana mimi na unaweza kula na chochote kile upendacho au hata yenyewe tu.
Mahitaji ni cabbage yenyewe, pilipili hoho nyekundu, carrot (hii nimeongeza mwenyewe), kijiko kimoja cha sukari, kijiko kimoja cha mafuta ya kupikia (ya alizeti/zeituni kama unayo),siki (vinegar) kiasi upendacho na pilipili manga (black pepper...samahani kama nimekosea kwa kiswahili) iliyosagwa kidogo.
Ukishakatakata kila kitu una-steam cabbage kwa dakika zisizozidi 5 maana hazitakiwi kuiva .Baada ya hapo unaziweka kwenye chombo ambacho utapenda kuchanganyia...kisha weka viuongo vyako vyote pamoja (vinegar unaweza kuweka kidogo kwanza na kuongeza baada ya kuonja na kuona kwamba unahitaji kufanya hivyo) alafu unavichanganya. Ukisharidhika funika vizuri alafu weka kwenye jokofu na itakua tayari kuanzia masaa manne baadae na kuendelea.
Aina nyingine ya salad ni hii (sina jina) unachanganya cabbage zilizokwisha katwakatwa pamoja na carrot zilizokwanguliwa.Unanyunyuzia chumvi alafu unaweka kikaangio chako jikoni....weka mafuta kidogo sana na uache kikaangio kipate moto kabla ya kuweka cabbage yako. Ukiweka cabbage hutakiwi kuifunika wala kuiacha jikoni muda mrefu...geuza geuza kwa dakika chache zikianza kulainika tu unatoa jikoni (hazitakiwi kuiva) kisha ziache zipoe kidogo. Zikishapoa nyunyuzia limao kidogo tayari kwa kula.Inanoga sana kula na pilau.
Cabbage soup.....Unakata cabbage vipande vipande, unachanganya na viungo vingine upendavyo (hoho, pilipili, vitunguu, viazi, vitunguu swaumu, nyanya n.k) alafu unavichemsha pamoja (nzuri sana kama uko kwenye DIET).
Kama ulikua hupendi cabbage jaribu kuitengeneza tofauti kwa namna tofauti na ile uliyozoea uone kama nayo hutoipenda.
Be blessed ....and stay blessed!! L.I.S
No comments:
Post a Comment