Thursday, September 1, 2011

Kusaidiana na kupeana moyo....

Behind every successful man is a great woman/Behind every happy woman is a wise man.


Siku zote baba huchukuliwa kama kichwa cha familia na mama ndiye shingo.Shingo inaweza kuelekeza kichwa popote inapotaka, ila ikitokea kichwa kikawa kizito sana itasababisha shingo ielemewe kitu kinachoweza kupelekea shingo kuvunjika.Hivyo hivyo shingo nayo ikiwa lege lege sana inapelekea kichwa kuanguka.


Hivyo basi....kina kaka/baba wasaidieni kina mama kwenye majukumu yao mnayoyaita ni ya wamama ili wasizidiwe sana.Enzi za kusema kulea watoto na shughuli za nyumbani ni za mama tu zimepitwa na wakati.Usiwe mzigo wa kumfanya mwanamke ajutie kukufahamu au aishie tu kuona wenzake wakifurahia maisha, msaidie mwenzako ili mwisho wa siku awe na nguvu za kukusaidia na wewe kwenye majukumu yako.Kusaidiana hakuishii hapo tu....hata kitu kama kupunguza pombe na kumsikiliza/kufuata ushauri wake iwapo una tija ni kumsaidia pia.


Kwa kina dada....wazungu husema ''Behind every successful man is a great woman'' choose to be that woman!Maana sisi kama wanawake(shingo) tuna nafasi kubwa sana katika maamuzi yanayopelekea mafanikio au maanguko ya wanaume.Kumkejeli mwenzako kwa maneno kama ''we ni mwanaume suruali'' ''huna maana '' na mengine kama hayo haifai.Kama angekua hayo yote usingekua naye!Mpe moyo linapokuja swala la kujiendeleza na kwenye maisha yote kwa ujumla...kumkatisha moyo kwa maneno kama '' huwezi kumfikia fulani...ana pesa sana yule'' ''kazi yenyewe unayofanya hata hailipi vizuri'' n.k kutampunguzia kujiamini.Katika watu wote wewe (kama mke, dada, rafiki, mpenzi, mwenzi, mama yake n.k) ndo unatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kumpa moyo na kumuaminisha anaweza na sio kumponda alafu unabaki kushangaa mbona  fulani ana mafanikio zaidi ya huyu wa kwangu wakati hawakua mbali sana.


Mwisho....furaha ya kila mmoja wenu inamtegemea mwenzake kwahiyo heshima iwepo(kupeana na kulindiana)..mapenzi ya dumishwe..kusameheana na kuombana samahani kupewe kipaumbele.. kusifiana na kukosoana kistaarabu nako kusikosekane!!All in all usimtendee mwenzako usiyopenda kutendewa(furahisha kufurahishwa...heshimu kueshimiwa.)


Be blessed ...and stay blessed!
L.I.S

No comments:

Post a Comment