Hi guys!
I was inspired to write this article by a friend so a lot of thanks to her.
Na hii ni maalumu kwa wasichana wenzangu!!
Kutoka kwa msichana mmoja kwenda kwa mwingine naanza kwa kusema TAMAA NI MBAYA.

Mwenyewe unaweza ukaona hamna tatizo lolote ikiwa na wewe unamtumia ila jiulize hivi...siku ukikutana na ambae atakutumia bila wewe kutarajia/kutaka ama kupenda kwa mfano KUKUBAKA ama tu ukalazimika kuwa katika mahusiano na mtu ambae pengine ni mgonjwa ukaambukizwa je utajisikiaje?! Probably not good. Alafu ukiachia mbali hisia zako unajua madhara ambayo unaweza ukapata kutokana na hicho kitendo?! Kuna magonjwa ya zinaa..mimba ambayo hukutarajia tena ya mtu ambae hukuchagua kushiriki nae mapenzi..kuathirika kisaikolojia n.k
Hasara ni nyingi hivyo jaribu/jifunze/jitahidi kushinda tamaa zako. Kama wewe mwenyewe huwezi kununua chips kuku au jeans unayoipenda kwa pesa yako mwenyewe au ya kupewa na watu wako wa karibu (ndugu..jamaa na marafiki) achana nayo. Hivi vitu havikimbii...hata baada ya miaka ishirini bado vitakuwepo tu.Kwahiyo tumia muda wako mwingi kujituma shuleni/chuoni kama bado unasoma au kazi kama unayo ili upate mafanikio ambayo yatakuwezesha kujiridhisha wewe na nafsi yako bila kulazimika kumtegemea mtu mwingine.
TAFAKARI.....JITUME!!!
Be blessed ....and stay blessed!
LI.S
Natumai wamekusikia!!
ReplyDeleteLIS, thanks for writing this. naomba ruhusa ya kunakili kwa ajili ya wapwa zangu.
ReplyDeletewakati wmingine sio kama wasichana hawana hela ya kujinunulia hizo chips,ni tabia tu ya kupenda mteremko. na ugonjwa umewapata hata wakaka! lets go back to the roots, rape will destroy ur future!
asante tena kwa kazi nzuri,always!