Saturday, August 27, 2011

What good are GREEN PEAS for...?

Owwkeyy...
Kila mara nitakua najitahidi tufahamishane uzuri wa vyakula mbalimbali ambavyo kwa wengi wetu havina kipaumbele sana. Pia nitakua nashea nanyi namna tofauti ya kuvipika vyakula hivyo ili kuongeza hamu/msukumo wa kuvila.
Leo tunaanza na green peas.....

Faida zake :
1. Zinapunguza cholesterol kwenye damu.
2. Zinaweza kusaidia kupunguza uwezekano wa kupata saratani (cancer) za aina
zote kutokana na kua na kiasi kikubwa cha Vitamin A na C.
3. Zinaweza kusaidia kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo na stroke.
4. Zinasaidia kupunguza hatari ya kuzorota kwa seli kunakoweza kuhusiana na umri.
5. Zina madini ambayo ni muhimu kuimarisha afya ya mifupa.
6. Zina madini ya chuma ambayo yanaweza kusaidia kuepuka upungufu wa damu
mwilini (Anemia)

Kama inavyoonekana hapo juu faida ni nyingi..ila sasa wangapi kati yetu hua tunazila? Nna uhakika sio wengi ukilinganisha na wasiokula kwakua nimeona kutoka kwa watu wanaonizunguka. Na ukweli ni kwamba hata mimi nilikua sili (kwakua nilidhani sizipendi) miaka
ya nyuma. Ila ukweli ni kwamba uandaaji wake ndio ambao haukunivutia.


Kuchemsha : Waweza zichemsha tu na chumvi (au kama zimegandishwa unapasha) na kuzila pembeni ya chakula chochote upendacho.

Unaweza ukachanganya kwenye mboga e.g kuku au nyama.

Unaweza ukatengeneza supu.Baada ya kuzichemsha unaziponda ponda kisha unaweka maji/maziwa na viuongo vingine upendavyo (vitunguu swaumu, black pepper, curry, binzari
n.k) kuongeza ladha.

Lastly my favorite...zilizochanganywa na wali pia sambusa.

Hizi napenda sana kwakua zinakua na ladha zaidi.Kwa kawaida hua baada ya kuzichemsha pamoja na carrot nazikaanga na vitunguu swaumu, binzari, pepper na curry kidogo kabla ya kuzichanganya na wali.

Pia waweza kuweka kwenye sambusa au aina nyingine yoyote ile ya pastry.

Sasa natumaini kuwa wale ambao walikua hawali kwa kutopenda ama kutojua umuhimu wake mtaanza sasa.




Be blessed....and stay blessed!
L.I.S

1 comment: