Wednesday, October 19, 2011

Ukishikwa.....

........shikamana!


Inashangaza kweli wakati mwingine jinsi watu wanavyoBEHAVE kwenye mahusiano.Wengine utakuta wanaendekeza KIBURI...wengine KUDEKA...wengine KULALAMIKA...KUGOMBA kila saa n.k tena bila sababu ya msingi.

Vyote hivi vikizidi kwakweli vinaweza kuvunja mahusiano maana INABOA/CHOSHA...kuna mtu unakuta hata akikosea yeye samahani mwiko.Hata ukimuwia mpole japo ye ndo mwenye kosa inakua bado haitoshi....yani kiburi chake ndo kinamtawala.
Wale walalamikaji nao yani utadhani ulimwengu mzima kabebeshwa yeye....kila saa kama anataka kulia..kila kitu ye ni kama anaonewa.Hata akifanya kosa kulia atalia yeye ...na kubembelezwa atabembelezwa yeye.Hawa wadekaji maarufu ndo kabisaaa...mtu kadri unavyombembeleza ndivyo anavyozidisha!Yani utadhani mashindano...mpaka mwisho wa siku mtu unaamua kumpotezea tu!

Nnachosema ni kwamba...mapenzi sio kukomoana jamani!Kila kitu fanya kwa kiasi!Wapenzi/wenza hawatakiwi kua na ushindani...labda kama mnashindana kuonyeshana mapenzi na sio nani kinara wa kulalamika au nani mwenye kiburi zaidi ya mwenzie!Hivyo basi ukishikwa shikamana...ukielezwa elewa...ukipendwa pendeka...ukiheshimiwa heshimu na heshimika pia!

Be blessed and stay blessed!
L..I.S

4 comments:

  1. Nimatumaini yangu hujambo and misukosuko ya kila siku. Jamani iko wapi hadith ya Zawadi? Mbona unatuboa hivyo?

    ReplyDelete
  2. Duh!!!Haya bana muendelezo tayari...pole kwa kuboreka!!!

    ReplyDelete
  3. Kuna tofauti kati ya mapenzi ya kusomea na mapenzi ya kuzaliwa.. Mapenzi ya kweli..yaani hayajali sura, hayana kushindana, hayana kuonyeshana ubabe ,hayana kuhisi hupendwi, hayana ubishi usio na msingi etc.. Ni amani moyoni na kufanya unachoona kinafaa bila kigezo cha kusubiri fadhila, au malipo..

    ReplyDelete
  4. Anon uko sahihi kabisa.
    Sema nadhani ni ngumu kuyapata hayo siku hizi!!

    ReplyDelete