Thursday, August 25, 2011

Dondoo za mapenzi...



Mahsusi kwa watu wanaotarajia kuanzisha mahusiano thabiti na yenye malengo pamoja na wale ambao tayari wamo ndani ya mahusiano ya aina hiyo.

KWA WATARAJIA

1.Usidanganyike na muonekano wa nje au yale maongezi ya mwanzo.
Kila mtu hua mstaarabu siku za mwanzo hata wale ambao sio.

2.Usikimbilie kutangaza nia haraka.
Siku zote ni rahisi mtu kua muwazi kwa rafiki yake kuliko kwa mtu ambae anajua anataka mahusiano nae kwa hofu ya kumpoteza.Tumieni muda wakutosha kufahamiana kama marafiki kabla hamjajiingiza kwenye uhusiano wa kimapenzi.

3.Uliza maswali kuhusu vitu ambavyo ni muhimu sana kwako.
Kwa mfano kama ni mtu wa familia au sio taka kujua mawazo yake kuhusu watoto hii itaepusha migongano isiyo ya lazima hapo baadae.

4.Penda kujua malengo yake ya baadae.
Hii itakuwezesha kugundua ni mtu wa aina gani...kama ni mpenda maendeleo,mtu wa starehe tu n.k.

5.Kua muwazi.
Hii inakwenda kwa pande zote...kuna vitu ambavyo ukimwambia mtu ni vidogo sana ila ukificha vinakua kwa vile tu ulifanya siri.

6.Hakikisha uwezo wenu wa kuelewa unaendana.
Hapa siongelei darasa ila mnavyokua sambamba kwenye maongezi ya kawaida tu yasiyo hitaji degree.

7.Onyesha misimamo yako hata kama unaona ni migumu kueleweka.
Ni vizuri mtu akikubali/taka kujiingiza kwenye mahusiano na wewe awe akijua atakua na mtu wa aina gani.K.m kama hupendi nguo fupi,mwanamke/mwanaume mnywaji wa pombe, mvuta sigara n.k sio unasubiri mpaka mue pamoja ndo muanze kuzozana.

8.Hakikisha kuna vitu mnavyoshabihiana.
Ni muhimu mkiwa na vitu mnavyoweza kufanya pamoja...iwe ni kuangalia movie ama kutembea nyakati za jioni inasaidia kuimarisha ukaribu wenu kuliko kila mtu kwenda na njia yake.


KWA WALIOMO NDANI

1.Mheshimu mwenzako.
Heshima ni kitu kidogo sana kutoa ila kikubwa kwa anaepokea.Kua muangalifu unavyomwongelesha na kumfanyia mwenzako pindi muwapo na watu wengine.

2.Kua muelewa na mvumilivu.
K.m kama mlikua mmepanga ama kuahidiana kitu fulani alafu hakijafanyika usianze kwa lawama...ohh hunipendi..mara hunijali!Omba sababu na ukipewa elewa.Kama hakikufanyika leo kitafanyika kesho....dunia haikimbii!!

3.Msome mwenzako.
Ukijua tabia za mtu ni rahisi sana kumuelewa na kukidhi mahitaji yake.K.m ukijua mwenzi wako anahitaji nini pindi anapokasirika...nafasi ya kutuliza hasira ama kubembelezwa papo hapo itasaidia kutokuongezeana hasira kwa kumfanyia kile ambacho sicho anachohitaji.

4.Kua mwepesi wa kuomba samahani.
Usipende kujikweza...kujishusha kidogo kwenye mahusiano haimaanishi wewe ni duni.

5.Kua msikilizaji zaidi ya muongeaji.
Kuna wakati mwenzi wako anakua anahitaji kutoa yaliyomo moyoni mwake tu....iwe ni hasira ama furaha bila kuingiliwa na ushabiki ama upinzani kwahiyo soma alama za nyakati.

6.Onyesha kujali.
Wakati mzuri kumwonyesha mwenzako unamjali ni pale anapokua na wakati mgumu...iwe ni kifedha..kiafya...kikazi na mengineyo.Sio lazima umpe pesa kama ndicho anachohitaji...ama kumpiga mtu ngumi kama ni swala la ugomvi....maneno mazuri ya faraja...kumuonyesha uko mapoja nae na kwamba unaumia anapoumia yeye inatosha kabisa kumpa mwenzako ahueni.

7.Kua msiri.
Jiheshimu wewe pamoja na mwenzi wako.Matatizo yenu ya ndani sio yakuanika nje kila anaepita aone.Inapotokea mmekosana sio mwenzako akitoka tu kwa hasira na wewe unachukua simu ama mguu huyo mpaka kwa shoga na shangazi wote wajue leo kwako kuna kauogomvi.Na sio hata mambo madogo tu utake msuluishwe na mtu wa nje...malizeni humo humo ndani kwenu.

8.Wivu.
Wivu ni mzuri katika kupendezesha mahusiano ila ni zaidi ya kero pale unapozidi.Kua na kiasi....

9.Mpe nafasi yake.
Kua pamoja ndani ya mahusiano haina maana mfuatane pamoja kila upande wa jiji...kumbuka yeye ana marafiki zake na wewe una wako na sio kila unachofanya lazima na yeye afanye!

10.Imani.
Iwapo mtu hajakupa sababu ya kutokumuamini..muamini.Inakera sana pale mtu anapoonyesha wasiwasi na wewe iwapo hujafanya chochote kusababisha hilo.Pia jiamini wewe mwenyewe kama wewe...unapendwa wewe...unathaminiwa wewe...sio hata salamu tu ikitolewa kwa mwingine unaanza kuwaka.

11.Kua mkarimu.
Kua mkarimu kwa ndugu na marafiki wa mwenzi wako.Sio lazima mdogo wake umlipie ada wewe...ama umpelekee mama yake gunia la mchele, kitendo cha wewe kumsukuma kufanya hivyo iwapo atakua anajiuliza afanye au la inatosha kuonyesha upo upande gani.

12.Usiwe na kiburi.
Kiburi hakijawahi kujenga popote.Kununa kwa muda mfupi kunaeleweka na kunakubalika iwapo umekorofishwa.Ila kususa chakula....kuhamishana chumbani na kunyimana unyumba havijengi bali vinabomoa.Ndo mwanzo wkutafutiwa msaidizi.

13.Mwisho kabisa usisahau KUSHUKURU na KUTOA SIFA kila mara.
Kumsifia na kumshukuru mwenzi wako kila mara itamfanya ajihisi anapendwa na itamfanya afurahie kua karibu na wewe tofauti na mtu ambae anatoa malalamiko tu.

Be blessed....and stay blessed!
L.I.S

1 comment: