Friday, October 28, 2011

Zawadi sehemu ya 7

Poleni kwa kusubiria sana mwendelezo.....

Kwa dakika nilitamani ningekua na uwezo wa kusoma mawazo ya baba nikajua nini kilikua kinaendelea kichwani kwake .Maana aliyofanya pale wodini yalikua nje ya matarajio yangu kabisa na hata nilipojaribu kufikiria nini kilichosabisha kile nilichoshuhudia sikufanikiwa. Nilidhani labda amechanganyikiwa, lakini hakuonekana kama mtu aliyechanganyikiwa bali mtu mwenye hasira zisizodhibitika.

Pamoja na kwamba baba hakusema neno baada ya zile purukushani hasira zake haziokuonekana kupungua. Wale waliomshika walimuomba watoke nje kidogo nae hakukataa. Akanitazama kwa jicho kali kisha akaongozana nao na kutoka nje ya wodi tuliyokuwamo. Kitendo cha kubaki pale chumbani mwenyewe hakikunipa unafuu bali kilinifanya niogope kile kilichokua kikiendelea. Nilitamani mtu mwingine aje mle ndani ili nijuzwe kilichokua kinaendelea ila haikua hivyo. Mawazo ya kuchomoa dripu niliyokua nimechomekewa mkononi mwenyewe ili nitoke nje yalinijia ila sikuthubutu.


Dakika zilipita mpaka pale mama alipoingia mle ndani na kuupa moyo wangu nafuu. Sikusubiri hata afike karibu yangu kabla ya kumrukia kwa maswali. ‘Mama nini tatizo? Mbona baba yuko vile? Nini kinaendelea?’’Nilimuuliza kwa mpigo huku nikimtazama kwa shauku. Badala ya kunijibu kama nilivyotamani alisogea karibu yangu akanitazama kwa muda. Macho yake yalikua mekundu kuashiria ametoka kulia, yalionyesha huzuni kana kwamba nafsi yake ilielemewa na mzigo wa habari mbaya. Kadiri alivyoendelea kunitazama ndivyo wasiwasi wangu ulivyoongezeka, nilikosa hata ujasiri wa kuendelea kumkodolea macho na kuangalia chini. Kama kawaida yangu nikaanza kutafuna kucha zangu za mikono , kitu ambacho nilifanya kila nilipokosa na kujihisi mwenye hatia. Kwa wakati ule sijui kwanini nilijihisi mwenye hatia, sikujua kilichokua kinaendelea au ni kwa namna gani nilihusika ila nilihisi nna hatia.

Zawadi mwanangu, Zawadi! Kwanini umeamua kuniabisha kiasi hichi lakini??’’ alisema mama kwa sauti ya kutetemeka. Bado sikua najua alichokua anaongelea hivyo sikujua nimjibu nini. Nilimtazama kwa wizi na kurudisha macho yangu chini mara moja kwa woga wa kuyakutanisha na yake. Alipoona nimegeuka bubu aliendelea kuongea huku machozi yakianza kumchuruzika. ‘Yani…..arrrrrg!!Nashindwa kuamini kabisa kwamba wewe Zawadi umeweza kunitenda kiasi hichi''

Mama alisogea na kukaa pembeni yangu kitandani, mkono wake wa kushoto akiwa ameulaza kwenye mapaja yake. Mkono wa kulia alikuwa ameshika ukingo wa kanga akifuta machozi ambayo yalikuwa yanatiririka kama maji. Nilijisikia uchungu kwani sikuwahi kumuona mama katika hali kama hiyo na nilijua kabisa lolote walilokuwa wanalizungumzia juu yangu lilikuwa ni kubwa sana.

Akili yangu ilikuwa inanizunguka na kunifanya nijisikie kizunguzungu. Nilitamani kumbembeleza mama na kumwomba msamaha lakini sikujua nianzie wapi na ni kwa kosa gani. Nilihisi donge likinikaba kooni na hamu ya kulia ikinijia. Pasipo kujijua nilihisi ubaridi wa chozi ukidondoka kwenye mashavu yangu.

"Mama kwani nimefanya nini mama" niliuliza huku nikiwa na kwiki. Kwa kweli sikujua kabisa. Kitu pekee nilichokifikiria labda ni mimi kwenda kwa Mwalimu au labda wamehisi nilikuwa na uhusiano usiofaa.

"Mwanangu umetuabisha, tutatokea wapi sisi" alisema mama kwa manung'uniko. Na mama alikuwa ni mnung'unikaji maana akinung'unika unaweza kuhisi dunia nzima inagubikwa na giza la majonzi na mvua ya uchungu kunyesha kama machozi ya kilio cha dunia.

"Niambie basi mama, nimefanya nini? Baba kanijia juu na wewe sasa unalia, miye sijui mama pleaseeeee niambie nimekosa nini mama" nilianza na miye kulalamika kwa uchungu na hasira kidogo. Nilikuwa nasema bora waniambie nijue kosa langu ili kama ni kuomba msamaha basi niombe msamaha yaishe. Sikutaka kuendelea kuwa katika hali ya kutokujua wakati wengine wakiwa tayari wanajua. Mama aliinua macho yake kuniangalia, alitaka kusema kitu ila alishindwa. Alivuta pumzi na kujifuta tena machozi. Aliniangalia tena kwa macho yake yenye huruma lakini yaliyojaa maswali na fedheha. ''Zawadi....kwanza naomba uniambie huyo mwanaume uliye na mahusiano nae ni nani.'' Mungu wangu...kusikia vile moyo wangu ulipiga paaah nikahisi unaelekea kupasuka. Akili yangu ilifanya kazi ya haraka kuchakatua nilichosikia, ''Amejuaje?Nani kwamwambia?Baba, ohhh God kumbe ndicho kilichomfanya baba awe vile??'' Pamoja na kwamba swali langu kuhusiana na baba lilipata jibu, maswali yaliongezeka na sikujua namna ya kuyapatia majibu.
Bila kumtazama mama moja kwa moja nilijikakamua kumjibu kama vile sikujua anachoongelea, '' Mi sija.....sina mahusiano na mwanaume yeyote mama.'' kigugumizi cha ghafla kilidhihirisha hofu niliyokua nayo. Nilitamani ningekua na uwezo wa kutoweka pale kukwepa mazungumzo yale ila bahati hiyo sikua nayo.

Mwalimu!Nilikua sijamfikiria hata kwa sekunde tangu sakati lile lilipoanza. Yote yaliyotokea baada ya yeye kuondoka yalishughulisha akili yangu kiasi kwamba hata sikunotisi kuwa ilikua imepita muda mrefu sana tangu aondoke wakati aliahidi kutokawia. ''Mama kweli mi sijawahi kuwa na mwanaume.'' nilikazia baada ya kuona mama amekaa kimya tu huku akinitazama. Ni kama vile alikua akinizungumzisha kwa macho , kunijulisha kwamba alikua anajua kwamba namdanganya. Seriously though, ningefanya nini?Kumwambia ukweli kulikua nje ya uwezo na matakwa yangu kwa wakati ule. Besides, nilikua naomba Mungu niweze kuwashawishi waweze kuniamini mimi na hayo waliyoyasikia wayapuuze kama maneno ya mtaani tu japo nilijua kutagua na ugumu ukichangia na kwamba sikujua habari hizo wamezipata wapi.
''We mtoto wewe, usije ukanifanya mimi mpumbavu ehh!!Sijazaliwa jana unajua?'' Nilishangazwa na mabadiliko kwenye sauti ya mama, alionyesha hasira kitu ambacho sikua nimezoea. ''Uanze kusema ukweli sasa hivi kabla baba yako hajakushughulikia.''
''Mama niamini sijafanya chochote, kweli vile nakwambia!!''nilimjibu kwa ujasiri wa kulazimisha.
''Yani wewe mtoto wewe, lini umekua muongo hivyo??Unataka kuniambia hiyo mimba uliyonayo ni muujiza ehh??'' Mama alisema kwa hasira huku akiinuka kutoka pale alipokua amekaa, mkono mmoja kiunoni na mwingine ukikuna kichwa chake kilichokua kimefunikwa na nywele fupi za wastani na kuzunguka mle wodini kama mtu aliyekua akitafuta mlango tofauti na ule uliokuwepo.
Haki ya nani niliposikia neno mimba nilihisi kajoto ka ghafla kwenye mapaja yangu. Mkojo ulinitoka, moyo ulinipasuka kwa mara ya pili na tumbo lilianza kunikata ghafla.Nilihisi mapigo yangu ya moyo yameongezeka maradufu, kuna wakati hata nilihisi nayasikia. Nilitumia mkono wangu wa kulia kufuta jasho ambalo halikuwapo usoni mwangu, kwa kurudia rudia mara kadhaa huku niking'ata midomo yangu ya chini kwa nguvu bila kujali wala kuhisi maumivu.Matokeo yake nilikuja yaona baadae.

Sijui nilitaka kusema nini ila nakumbuka kufungua mdomo wangu mara kadhaa katika jitihada za kusema kitu lakini sikufanikiwa kutoa hata sauti. Nilijua natakiwa kumwomba mama radhi ila sikujua pakuanzia hivyo nikabaki nawaza nianzeje kuongea na mama.Nilichotaka kwa wakati ule ni kujua kwa hakika kama kweli nilikua na mimba ama walikua wananitania tu, japo nilijua kwamba uwezekano wa wao kua wananitania ulikua karibu na sifuri bado sikuacha kuomba muujiza utokee waniambie haikua kweli au nizinduke toka usingizini maana yote yaliyotokea siku ile hayakua tofauti na nightmare ambayo hata wewe usingependa iendelee.

10 comments:

 1. Jaman we mrembo uusicheleweshe tena uhondo mmmh! Maana hadith nzuri sbb iko karib na ukweli wa yanayotokea kila day ndan ya Tanganyika... Umegusa nyoyo zetu bibie. Du Mungu awe pamoja nawe

  ReplyDelete
 2. Asante mpenzi...
  Ntajitahidi...tuombeane uzima tu!!

  ReplyDelete
 3. Jaman c umalizie huo uhondo mpendwa, me lov it!

  ReplyDelete
 4. kweli kabisa usicheleweshe tunatamani iwe kwa mfululizo asante

  ReplyDelete
 5. Dah.....!!! Hii story inanoga kila kukicha. Halafu umegonga mulemule kabisa, ni ngumu kuadmit upesi hata kama binti anajua tatizo litakuwa lilitokea siku flani na flani. ukweli mtupu, haya ndo mambo yaliyopo ktk jamii yetu. KILA LA KHERI BIBIE.......NASUBIRIA MUENDELEZO!!

  ReplyDelete
 6. Haki ya nani we dada Fundi,yaan mi naamini hata shigongo hakuwezi...yaan hadith yako ina uhalisia ktk maisha ya kawaida.Labda nikupime na level za kina Ben R mtobwa,E.A.MUSIBA au RAJABU HAMIE
  Daah upo juu sana mshkaji wangu.

  ReplyDelete
 7. Anon hapo juu kabisa ntajitahidi usijali!!

  Happy asante mpenzi...

  Anon wa mwisho asante..bichwa limenivimba wewe.Ngoja nikaze buti nisije nikawadisappoint.

  Love you all....thanks for the support!!!
  L.I.S

  ReplyDelete
 8. so nice! you get the talent dear! keep it up! When you publish the hard copy I will be the first one to have it. Kazi nzuri sana.

  ReplyDelete
 9. raphael
  kwakweli nimeguswa na story yako na imenifanya kuisoma kuanzia saakumi up to saa kunambili ongela sana. kwa ushauli wangu unge tayalisha kitabu na kuvipeleka mashuleni ili wadogo zetu
  wajifunze kwani siwote wanaopitia hadhi kama izi zenye mafundisho kwenye mitandao .

  pili:kwa wazazi,kama hi hadith inge wafikia wazazi ni mafundisho tosha inaonyesha jinsi ngani wazazi wasivyo kua kalibu na watoto wao wakike ata kuwapa elimu ya kutosha ya uzazi.kwani walimu wa siku izi awako makini na wanafunzi.
  tatu:nakupa ongela nimevutiwa na blog yako katika blog zote za hapa tz wewe uko to fauti .kawni wengi wanazungunzia starehe badala ya kuangalia jamii inakwenda wapi.

  to end: yangu ni ayo tu you make my day to so thinkful

  ReplyDelete
 10. duuh kweli nilikuwa namic hichi kitu nilivvokuwa siko hewani liz mway,thanx much i love the story thou inaanza kusikitisha.big up sana mamii

  ReplyDelete