Sunday, October 30, 2011

Wakatisha tamaa...DOWNERS!

Downers....
...That's what I call the people that are constantly trying to put others down.

Watu kama hawa wako kila mahali, majumbani, mashuleni, makazini na hata mitaani.Wanawashushia wenzao ari ya kusoma, kutafuta maendeleo, kufanya kazi, kukuza na kuendeleza vipaji vyao kwa sababu ya madhaifu yao wenyewe au woga wa kuwaona wengine wakifika mbali.

Muda sio mrefu nilitokea kuangalia kipindi cha mashindano ya kuimba, kabla ya kuimba dada mmoja (umri miaka 37 kama sikosei) akawa anaelezea kwanini imemchukua muda mrefu kujaribu bahati yake. Alikua na mpenzi ambae kila akiimba alikua anamwambia hana sauti nzuri na maswala ya kuimba hayawezi kumfikisha popote kwasababu hana kipaji. Dada wa watu alisikia hayo maoni so many times mpaka na mwenyewe akaanza kuamini kwamba ni kweli hana kipaji japo wakati anakua aliamini anacho. Akapoteza kujiamini mpaka alipokuja kuachana na yule bwana na ndio akaona aende kwenye hayo mashindano.
Honestly yule dada alipoimba tuchozi tulinitoka....pamoja na watu wengine wengi tu waliokuwepo kweny hicho kipindi.Her voice was simply AMAIZING.....

Wapo watu wengi sana wanaonyang'anywa kujiamini kwa namna hii..wakubwa kwa wadogo.Wakati mwingine hata mzazi anaweza akachukua nafasi hiyo ya kumshusha mwanae...yaweza isiwe kwa makusudi bali kwa yeye kuamini kwamba mwanae hawezi hicho anachojaribu ila inatokea na inaathiri.


So next time ukisikia mtu anakwambia ''huwezi hichi...huwezi kile'' usichukulie hayo maneno kama sheria. Usikubali kuaminishwa huwezi wakati unaweza...hutofika mbali wakati matumaini yapo...WASHANGAZE watu waliodhani hutofika, hutoweza kwa kupigania na kufikia malengo yako.

Jifunze kutofautisha criticism na discouragement.
..Criticism imejikita kwenye kujenga na kuboresha zaidi. Kukupa moyo na kukuimarisha...UKIPEWA CHUKUA NA TUMIA VIZURI KWA FAIDA YAKO.
..Discouragement imejikita kwenye kubomoa msingi wa kujiamini kwenye mambo au jambo fulani. Kukuonyesha kwamba huwezi na hata ufanye nini hutoweza .HII USIRUHUSU IKUTAWALE.

Kama wewe ni mzazi...jitahidi kumkosoa mwanao pale inapobidi ili kumjenga (critisism is good ) ila usimkatishe tamaa.
Kwa wengine wote....usiruhusu madhaifu yako...kutokujiamini kwako...chuki...wivu au hata mtazamo wako kuhusiana na maisha uathiri watu wengine. Kosoa kwa nia ya kujenga ...kama huwezi acha!!

Be blessed....and stay blessed.
LIS

3 comments:

  1. Good message!! Wengi tunapima matakwa yetu kwa kuangalia watu wengine. Ni vizuri kuchukua ushauri ambao watu wanakwambia, ufanyie kazi kwa kuuchuja na si kuuchukua kama ulivyo. Tushauriane kwa upendo na si kukatishana tamaa. Wasome watu ulionao na ujaribu kuwaelewa na uelewe pia the way wanavokuchukulia, usijiegemeze sana kwa mawazo yao, jaribu kuwa na your own ideas and think independently, kuwa makini na ideas zilizo popular sana, jenga imani yako mwenyewe........PENYE NIA PANA NJIA!! Barikiwa sana LIS

    ReplyDelete
  2. Asante dearest...right back at ya!!!

    ReplyDelete
  3. Ongera sana Lizzy kwa blog yako, keep it up Malkia and be Brave...

    X-Paster

    ReplyDelete