Saturday, August 27, 2011

Zawadi sehemu ya tatu...


Sehemu ya tatu...

Alinishika mkono wa kulia kwa nguvu na kunivuta ulipokua mlango wa chumbani. Bila kunitazama usoni aliuachia mkono wangu na kunisukuma kitandani , hapo ndipo akili yangu iliporudi. Nilijua nini alichokusudia kufanya na nilihitaji namna ya kuzuia kitendo kile.Kwa haraka niliinuka toka kitandani ili nitoke mbio ila sikupata mwanya huo maana mara hii baada ya kunisukumu alinikandamiza chini kwa mikono yote miwili. Mpaka wakati huo bado sikuelewa mabadiliko yale yalitokana na nini haswa. Macho yake yaliyokua yakinivutia mwanzoni yalinitazama kwa ukali, na kwa mara ya kwanza niliogopa kuangaliwa nayo.
“ Unaniumizaaa“ nililia kwa sauti ya chini. Hakuonekana kujali kwani ndio kwanza alinitazama kwa ukatili. “Malaya mkubwa wewe.“ alisema kwa gadhabu, “Huna shukurani kabisa. Unakula pesa yangu kumbe unaliwa na wengine huko?! Ngoja nikufundishe heshima kidogo“ alisema huku akiwa ameshika shati langu tayari kulirarua.

Machozi yalinitiritika sambamba na sauti ya vifungo vilivyoanguka sakafuni, vilivyogonga ukutani na pia sehemu ya kitanda.Alisogeza uso wake kifuani kwangu kama mtu anaechunguza kitu kisha akaupandisha taratibu.Midomo yake ilipokaribia yakwangu nikafikiria namna ya kumuondoa juu yangu, alipoikutanisha tu yangu na yake nilimng‘ata japo sio kiasi cha kumtoa damu!! “Mamaaa“ alilia huku akiruka kwa maumivu na kujilaza chali pembeni yangu huku akichunguza midomo yake kwa ulimi na mkono wake.Nikatumia mwanya ule kukimbia mpaka sebuleni na moja kwa moja nilielekea mlangoni.Mkono wangu ukiwa umeshika kitasa cha mlango tayari kuufungua nilihisi maumivu makali shingoni. Alinigeuza akanitazama kwa hasira kisha akanikokota tena mpaka lilipokuwapo sofa bila kusema neno. Alinisukuma kisha akanyanyua miguu yangu na kuiweka juu. “Sasa urudie tena ushenzi uliofanya uone ntakachokufanya.Hivi wewe unanijua au unanifahamu?!“ ......“Si nakuuliza wewe?!“ alinizodoa kwa kidole. Sikuweza kujibu maana kilio na kwikwi vilinitawala.
Kwa haraka nilifikiria kwamba hamna nnachoweza kufanya kujinasua toka mikononi mwake, na nilishajua kwamba nikileta ukorofi anaweza akanifanya chochote kile hivyo nilitulia na kuacha kilio changu kionyeshe hali niliyokua nayo.Alivua suruali yake huku akihema kwa nguvu baada ya kupandisha sketi niliyokua nimevaa mpaka kiunoni. Akashika nguo yangu ya ndani na kuivuta juu na kuiachia mara mbili alafu akaanza kuishusha chini.Niliinua miguu yangu juu usawa wa kifua chake na kuibana kwa nguvu zangu zote. “Umeshazoea huko alafu hapa ndio unataka kujifanya mgeni?!Embu usinifanye mpumbavu.“ kauli yake hiyo iliniingia. Sikujua amepata wapi mawazo hayo wakati alijua fika sikuwahi kuhusiana na mtu kimwili. Mwenyewe aliniambia na kunisihi nisikubali kufanya hivyo hovyo kwasababu nastahili zaidi ya kufanywa chombo cha matumizi na mwanaume yeyote yule. Hata yeye alikua tayari kunisubiria nimalize shule ili aweze kunifanya mkewe kabla ya kunijua kimwili. Iweje leo ......!Mawazo haya yalikatishwa mikono yake miwili kufanikiwa kuachanisha miguu yangu.

Sikuona sababu ya kumzuia tena, machozi nayo yalishaanza kukauka japo bado kwikwi zilikuwa nami.Nilifikiria kupiga kelele ila nani angekuja?!Sikujua kama majirani walikuwepo au hawakuwepo. Na hata kama walikuwepo, ingekuaje kama wasingehangaika kutaka kujua nini kinaendelea na kunisaidia?Si ningemkasirisha zaidi!?Japo kwa kutulia kungedhihirisha udhaifu wangu mbele yake sikua na ujanja. Kilichofuata pale yalikua maumivu makali ambayo nisingependa kuyakumbuka daima.Nilihisi kama mtu aliyekatwa na kisu sehemu laini.Niliweza kuachia yowe moja tu kabla hajaniziba mdomo na kuongeza nguvu na kasi kwenye kile alichokua akifanya.Nililia nikalia alafu nikalia tena.

Mishale ya saa kumi na mbili jioni niliondoka pale kwake nikiwa nimevalia shati ambalo halikua saizi yangu.Nilielekea moja kwa moja alipokua anaishi Ester.Kabla ya kufika kwao nilimtumia ujumbe kwa njia ya simu kumuomba tukutane Mwembeni .Giza lilishaanza kuingia hivyo sikua na wasiwasi wa watu kunishangaa nilivyokua nimevimba uso au nilivyokua natembea.Hata Ester hakugundua tofauti yoyote mpaka nilifika alipokuwepo sababu kulikua na mwanga wa taa ya chemli iliyowekwa juu ya kibanda cha mboga mboga. “WEWE!!! Mbona hivyo umefanyaje?!“ aliuliza kwa mshangao huku macho yamemtoka.Alisogea karibu na kuugusa uso wangu kuona kama nilikua nimeumia, nilitazama chini nisijue cha kumjibu. “Niambie basi, home wamekumaind?!“ aliuliza tena, mara hii nilitikisa kichwa upande kuashiria hapana. “Naweza umm ...kulala kwenu leo?!“ sikua nimetoa neno tangu kilichotokea kilipotokea hivyo nilishangaa sauti yangu ilivyokua imebadilika. “Hamna noma! Ntamwambia mama umekuja tumalizie kujiandaa kwa mtihani.“ maneno yake yalinipa ahueni, akanishika mkono na kuniongoza ilipokuwepo nyumba yao.

Tulizunguka uani na kuingia ndani bila kuzungumza, tulipofika kwenye korido aliita kwa sauti kumjulisha mama yake aliyekuwepo sebuleni kwamba nimefika kujiandaa kwa mtihani. Nashukuru Mungu umeme ulikua hamna hivyo sehemu kubwa ya nyumba ilikua imetanda giza isipokua sebuleni. “Hujambo Zawadi?!“ mama yake alinisalimu kwa sauti ya upole. Nilikohoa kwanza ili kulainisha sauti yangu kabla ya kumsalimu na kumjulia naye hali. “Alafu nyie sio mliseme leo mtapumzika kusoma?!Au ndo usomi wenyewe huo?!“ mama Ester aliuliza huku akicheka nasi tukamuunga mkono. Ghafla nilitamani yule ndio angekua mama yangu. Mpole, mrembo na siku zote alikua kama hacheki basi anatabasamu. Sikuwahi kumsikia akigomba au kumuona akiwa amekasirika. “Anyway , fanyeni mambo yenu chakula kikiwa tayari ntamwambia dada awaletee.“ alisema nasi tukaitikia asante kwa pamoja.

Haikua mara ya kwanza mimi kulala kwa kina Ester hivyo sikua na wasiwasi ntakavyojieleza nyumbani. Urafiki wetu watatu uliendelea hata nje ya shule na wote tulijulikana kwa kila familia ya mmoja wetu, na kipindi cha maandalizi ya mitihani tulipokezana kulala kwa kila mmoja ili tuwe tunasoma pamoja. Nilimpigia mmoja wa majirani zetu na kumuomba niongee na mama baada ya salam.
“Halo.“ mama alisikika.
“Mama, ni mimi.Pole na kazi.“
“Enhe muda wote huu uko wapi?!“ aliuliza bila kupokea pole yangu.
“Umm nilipita kwa kina Ester tukaanza kusoma mpaka sasa hivi ndo nashtuka.Nlikua nataka kukuomba kama naweza kulala ili tuendelee kusoma mpaka usiku.“
“Yani wewe mtoto wewe.Kwahiyo hizo ratiba zako huwezi kuweka wazi mapema?!Haya utajuana mwenyewe na babaako hiyo kesho ukirudi.“
“Asante mama, kesho basi.“ nilimalizia na kukata simu!

Kule chumbani kulikua na tochi kubwa iliyofanya kuwe na mwanga sana tofauti na ilivyokua sebuleni, hivyo nilimwomba Ester kama hatojali aizime au awashe mshumaa pekee.Tulikaa kitandani bila kuzungumza kwa muda kidogo ndipo apotaka kujua kilichonisibu.Nilimweleza mwanzo mpaka mwisho, alichofanya yeye ni kuitikia tu na kutoa macho mpaka nilipomaliza.
“Weeee! Kwahiyo akananiii?!“ “Mhuuu“ nilijibu bila kutoa neno.
“Pole mwaya!Umemwambia mtu?!“ aliuliza kwa tahadhari. “We ndo mtu wa kwanza kukwambia.We unadhani kwanini sikutaka kwenda nyumbani?! Nilivyovaa na huu uso sijui ningejieleza vipi.Mwenyewe nimejiona hapo kwenye kioo nikajiogopa!“ “Sasa utafanyaje?!“ alinitupia swali jingine. “Sijui.“ jibu langu lilikua fupi maana ni kweli sikujua nifanye nini. Kuwaeleza nyumbani sijui ningeanzia wapi. “Umm labda tukimwambia mama yangu anaweza kujua nini cha kufanya.“ alitoa wazo ambalo halikua baya sana kwa vile nilivyomjua mama yake ila sikua tayari kuelezea tena kilichotokea. “ Uhh uhh!!Labda kesho, ntafikiria.“
“Ok! Kwahiyo sasa hakusema kitu wakati unaondoka?!“
“Aliniomba samahani ila sikumjibu nikavaa zangu na kuondoka.Kanipigia sijapokea alafu akanitumia meseji kwamba atanitafuta kesho na anaomba nisimwambie mtu.“ nilimjibu kwa sauti ambayo ilianza kufanana na ile niliyoizoea.Hata hasira niliyokua nayo ilikua imepungua. “Kheeee!!Mshenzi kweli, yani kakufanyia hivyo alafu anakuomba samahani?!Kisa?!Ningekua wewe haki ya nani ningeshtaki awekwe ndani.“ maneno yake yalishapita mawazoni mwangu ila nilipotezea baada ya kugundua kwamba hata mimi ntakua matatizoni maana baba hatoelewa kabisa nilichokua nakifanya kwa mwalimu Samea mpaka yote hayo yakayokea. “Nimefikiria ila nyumbani wakijua baba sijui atafanyaje. Ohhh alafu unajua kwanini aliniomba msamaha?!Kwasababu alivyomaliza alikuta damu kwahiyo akajua sikua nimefanya mapenzi na mtu kabla.Kumbe alivyoona meseji za Jerry akadhani nimetembea nae.“
Muda huo huo Ashura alituletea chakula hivyo hatukuweza kuendelea na mazungumzo yetu. Nilishangaa kwamba niliweza kula karibu nusu ya chakula nilichotengewa, kwa muda nilihisi niko katika hali ya kawaida.

Be blessed...and stay blessed!
L.I.S

4 comments:

  1. Wow this is fantastic blog, I am gonna bookmark your blog!! You have earned Number one fan.
    Congratulation

    ReplyDelete
  2. u ar already bookmarked here! asante,hadithi nzuri ila the suspense is killing me LIS banaa, bring it onnnn!

    ReplyDelete
  3. @Kweli...thanks a lot mpendwa!!

    @King‘...be patient!!Muendelezo unakuja!!

    Thanks guys for visiting my blog!!

    ReplyDelete