Thursday, August 25, 2011

Mimi na wewe....

Siku kadhaa zilizopita nilikua nafikiria kitu nikajikuta naangalia mahusiano na ndoa kwa namna ambayo sikuwahi kabla. Mimi na wewe ni kama vipande vya puzzle ....you've got your share and I have got mine.Ukiviweka pamoja either unapata picha/umbo kamili ama hupati.




Kila mmoja ana shape na size tofauti.Inapotokea wewe kama puzzle umemchagua mtu ambae yeye kama puzzle hana shape zinazoendana na vipande ulivyonavyo ndipo matatizo na migongano inapoanza.Utajitahidi kunoa na kuongeza zile sehemu zisizofit vizuri kwako au kwake ila mwishoni unashangaa pamoja na jitihada zako zile sehemu zinapwaya na ukiendelea kulazimisha zinavunjika na kuvunjika.

So jambo la muhimu hapa ni kutafuta vile vipande ambavyo vinaendana na vyako.One that is complementary to yours....one that accomodates your needs.

Linapokuja swala la ndoa ndo kabisa umakini wa hali ya juu unahitajika.Hapa kinachofanyika ni kuvishikanisha vipande vyako na vya mwenzako kwa glue.Hata kama haviendani at first havitakua na jeuri juu ya glue....ila baada ya muda utashangaa huku kunameguka...na vikianguka tu vinavunjika vunjika.Ila kama vitakua vinaendana ni rahisi kustahimili mitikisiko na mianguko.Hata sehemu ikimeguka ni rahisi kuirudishia.Kwahiyo kuweni waangalifu....usichukue tu vipande ni vipande...

....bali tafuta vile vinavyokufaa!!

Kwa kuongezea.....

Wakati mwingine hutokea kwamba baadhi ya watu wanaona puzzle zao zinafit na baadae hazifit na wengine wanaoona hazifit na baadae wanashangaa sio kama ni miujiza au bahati mbaya vinakua vimewatokea.Bali hayo ni matokeo ya kutumia puzzle za MATAKWA yao kutafuta kile WANACHOHITAJI!!!

Kwahiyo wale wanaopata zinazofit wanakua wamepata kile wanachokitaka...ila baada ya muda mabadiliko yanakuja!Wanagundua kwamba walichotaka na kukipata sicho wanachohitaji!Hivyo hivyo kwa wale wanaodhani wamebahatika kuona muujiza mbele ya macho yao...mtu anakua ametumia puzzle za matakwa na kuona kwamba haziendani na za mwenzake.Ila kumbe zinaendana na mahitaji yake ambayo ni muhimu kuliko matakwa.

Na tatizo hapa ni kwamba wengi hua tunafikiria na kujua ni nini tunachotaka bila kujishughulisha kufahamu tunayohitaji!!!Ndio maana unakuta mtu aliwahi kukupa sifa za atakae kua mke wake baadae ila siku ikifika akakutambulisha unajiliza kama amesahau sifa zake zile au la!Sio kama anakua hajawaona wenye sifa alizotaka awali. Na wakati mwingine unakuta mtu anatamba sana mwanzoni kwamba mwenzangu ana kila NNACHOTAKA ila muda sio mrefu unashangaa akisema yule hakua size yangu au hakunifaa!Ukiangalia sifa zote alizotoa mwanzo kama ni uzuri/pesa/ndoa/ n.k bado viko pale pale!!

Be blessed...and stay blessed.
L.I.S

1 comment:

  1. LIS na mapenzi duh! tutasoma mengi NWY great job!

    ReplyDelete