Sunday, October 2, 2011

Wazazi wenza.....

Linapokuja swala la mahusiano/ndoa na watoto waliozaliwa kabla hua hatuachi kuongelea mama wa kambo na malezi ya watoto.Napenda kuongelea wamama tu maana wababa wengi hua hawana matatizo wawe wazazi kabisa au walezi(wale wa kambo) linapokuja swala la mzazi mwenza kua na mahusiano mapya au wale wa kambo kulea watoto wa mwenzie tofauti na wa mama!


Nwy mara nyingi wasiwasi hua unakua kwa watoto zaidi na malezi/uwepo wa mama wa kambo.Tunasahau kwamba hata yule mwanamke mpya anaweza akanyanyasika na uwepo wa watoto wasio wake pamoja na mama yao bila kusahau ndoa yake kuyumbishwa kama mti usio na nguvu dhidi ya upepo.Kama tunavyojua wakati mwingine au niseme baadhi ya wanawake hua na vinyongo..gubu..chuki kwa wazazi wenzao kwa kuachana nao...na kitendo cha mwanaume kupata mwanamke mwingine na kuoa hakiwi cha furaha kwa wote!Sasa wanawake wa aina hii wanaweza kutumia watoto wao kuyumbisha ndoa ya wengine pia kusambaza chuki.Ila muhimu hapa ni hili la kuyumbisha ndoa...kuharibu au hata kuondoa kabisa amani ndani ya nyumba ya mwanamke mwingine kwa kutengeneza mazingira ya kuwachanganya wapendanao!
Unakuta mwenye watoto anawatumia wanae kumuendesha mwanaume kama gari moshi kitu ambacho hakiwezi kumfurahisha mwenye mume.Yani kama aliyeolewa ni mwepesi wa kukasirika na kubugidhiwa ndoa inaweza ikaishia kuzimu.


Nakumbuka kuna mtu wangu wa karibu alipata shida sana kipindi cha mwanzo cha ndoa yake.Mwenye watoto alikua ni mkorofi sana na kila anachofanya anafanya kukomoa tu.Watoto amewahamishia shule ya kawaida ila ada anapokea ya shule ya international.Anawadanganya watoto wakubali kwamba wanaumwa ili amchune baba wa watu mpaka abaki mifupa tu.Ilikua kazi kweli maana unakuta mke alishataka/hitaji kitu akaambiwa pesa hamna bwana mwezi huu tufanye kitu flani alafu mwezi ujao tutafanya utakavyo...alafu mwenzie anapiga na kuagiza wala sio anaomba awe amepata maelfu kadhaa ndani ya masaa na anapata bila ubishi. Alilia mpaka baadae alipogundua kwamba sio kosa la mume wake...yeye tatizo lake ni mapenzi kwa wanawe na woga kwa yule mama.Ikabidi aanze kumshauri mumewe asiwe mwepesi wa kukubali kuchezewa na yule mama ndo mume nae akawa mgumu na kukataa kusukumwa kama mkokoteni!

Kwahiyo naomba niwaulize wababa wenye mtoto/watoto tayari..hawapo kwenye ndoa ila wanatarajia kuwa siku moja...mmejiandaa vipi kukabiliana na changamoto zitakazosababishwa na juhudi za wazazi wenza kutaka kuvuruga ndo zenu na kuwaondolea amani ndani ya nyumba????!

Binafsi naamini mwanaume akikataa kuchezewa na mzazi mwenza basi haitatokea...hivyo basi nawashauri muwe mnawapa wale mlio nao kipaumbele.Kama akiashiria kua kuna matatizo yanayosababishwa na mzazi mwenzio hakikisha tu haitokani na chuki kisha yafanyie kazi.Usikubali kuharibiwa ndoa/mahusiano yako kwa kisingizio cha watoto ambao mara nyingi hata hawahusiki bali wanatumiwa tu kama sababu.Usikubali kutumiwa wala kuchezewa....unaweza kufika mahali hata mahitaji mengine ya mtoto ukanunua mwenyewe usije ukageuzwa kitega uchumi.Kwa wamama ukijikuta kwenye situation kama hii jitahidi kua mvumilivu na mshauri wa mwenzio...pia jitahidi matatizo yatakayosababishwa na mama mtu yasizae chuki kwa mtoto!!

Be blessed and stay blessed.
L.I.S

No comments:

Post a Comment